" WAZAZI WAHIMIZWA KUCHANGIA CHAKULA SHULENI

WAZAZI WAHIMIZWA KUCHANGIA CHAKULA SHULENI


Na Mwandishi Wetu, KahamaWAZAZI wilayani Kahama, mkoa Wa Shinyanga wamehimizwa kuendelea kuchangia chakula mashuleni ili kusaidia kukuza kiwango cha elimu na kuwafanya wanafunzi kusoma katika mazingira bora na yenye utulivu. Wito huo umetolewa na viongozi wa chama na Serikali Mei 12, 2026 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha maendeleo ya kata ya Majengo kilichoongozwa na Diwani wa kata hiyo, Zacharia Soko, kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Samia iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.Kikao hicho kilihusisha viongozi mbalimbali wa serikali na chama, akiwemo Afisa Maendelo wa kata, Mtendaji wa kata, Mwenyekiti wa mtaa wa Sokola pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya maendeleo ya kata. Baada ya kikao hicho, viongozi hao walikabidhi mahitaji ya chakula shuleni na vifaa vya kupikia kwa shule mbalimbali zilizizopo ndani ya kata hiyo.Moja wa msaada huo uliokabidhiwa ni zaidi ya kilo 50 za mchele, maharage, sukari, mahindi kwa ajili ya unga wa uji pamoja na vifaa mbalimbali vya kupikia. Shule zilopokea msaada huo ni Shule ya Msingi Majengo, Shule ya Msingi Anderson Msumba pamoja na Shule ya Sekondari Samia.Akizungumza baada ya zoezi hilo la kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokola, Patrobas Privatus, alisema kuwa lengo la Diwani kujitolea mahitaji hayo siyo kubeba mzigo peke yake, bali ni njia ya kuhamasisha wazazi na wananchi kuwa na mwamko wa kuchangia chakula kwa wanafunzi ili waweze kusoma kwa utulivu zaidi.“Diwani wetu ameamua kuonyesha mfano kwa vitendo ili wananchi waone umuhimu wa kushiriki jukumu la kuwalisha wanafunzi mashuleni. Mtoto anapopata chakula anakuwa makini darasani na kufanya vizuri katika masomo yake,” alisema Privatus. mwenyekiti WA mtaaKwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Kahama, Laurent Nkwabi, aliwataka wazazi kumuunge mkono Diwani huyo ili kuhakikisha watoto wanapata chakula cha kutosha shuleni jambo ambalo itasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao katika mitihani yao.Alisema kuwa changamoto ya chakula mashuleni imekuwa ikichangia baadhi ya wanafunzi kukosa umakini darasani kutokana na njaa, hivyo ushirikiano wa wazazi na viongozi ni jambo la muhimu katika kuboresha elimu.Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Majengo, Sebastian Masonga, alisema chama hicho kinafurahishwa kuona viongozi wanaotekeleza ahadi zao kwa vitendo badala ya maneno.Masonga alisema Diwani huyo wa kata hiyo amekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia changamoto mbalimbali za wananchi likiwemo suala la chakula mashuleni na ukarabati wa barabara za mitaa.“CCM tunajivunia kupata kiongozi mwenyeye kuwajibika kwa wananchi wake. Haya yanayofanywa na Diwani wetu ni mfano mzuri wa uongozi wa vitendo. Tunawaomba wazazi waungane naye kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula na mazingira bora ya kujifunzia,” alisema Masonga karibu Wa CCM Majengo.Akizungumza katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Majengo, Zacharia Soko, alisema msaada wa chakula kwa shule ni sehemu ya ahadi alizozitoa kwa wananchi kipindi cha kampeni wakati akiwaomba ridhaa ya kuwaongoza.Alisema kuwa hadi sasa ametumia zaidi ya shilingi laki tano kununua chakula na mahitaji mengine kwa shule hizo za kata hiyo, huku akiahidi kuendelea kufanya hivyo kila mwezi ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula na kufanya vizuri katika masomo yao.“Niliomba nafasi hii ili niwatumikie wananchi wa kata ya Majengo kwa moyo wote. Nitaendelea kusaidia shule zetu ili watoto wapate mazingira bora ya kusoma. Elimu ni msingi wa maendeleo yetu,” alisema Soko.Aidha, Diwani huyo alisema kwa sasa anaendelea na zoezi la kukwangua na kukabati barabara zote za mitaa kwa kutumia fedha zake binafsi, ambapo ametenga kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila mtaa kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizizoharibiwa na mvua za masika.“Kwa sasa ninaendelea kukarabati barabara za mitaa kwa fedha zangu binafsi kwa sababu wananchi wanahitaji huduma bora za usafiri na usafirishaji. Barabara nyingi zilaharibiwa na mvua, hivyo lazima zirekebishwe kwa haraka zaid,” alisema.Katika hatua nyingine, Diwani huyo ameahidi kushughulikia tatizo sugu la mtaro mkubwa unaosababisha maji kuporomokea  kwenye makazi ya wananchi hasa kipindi cha mvua za masika.Alisema ataendelea kushirikiana na Wakala wa Barabara Mkoa wa Shinyanga (TANROADS) kuhakikisha madaraja makubwa yanakarabatiwa ili kusaidia kuelekeza maji hayo kwenda katika bwawa la Lyanzungu lililolopo Kata ya Mhongolo kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo cha umwagiliaji.Wananchi wa Kata ya Majengo walieleza kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na Diwani wao, wakisema zimekuwa chachu ya maendeleo katika eneo hilo huku wakitaka viongozi wengine kuendelea kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.Mwisho.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post