Balozi wa Italia nchini Tanzania, mheshimiwa Giuseppe Sean Coppola, ametembelea banda la TANESCO katika maonesho ya COPE yaliyofanyika katika viwanja vya VETA, Manispaa ya Songea, na kupongeza juhudi zinazofanywa na shirika hilo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wananchi.Akiwasilisha Kwa mgeni rasmi Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bertha Joseph Sahi, alisema shirika linaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuelimisha wananchi kuhusu faida za matumizi ya nishati safi, hususan matumizi ya umeme katika shughuli za majumbani na kiuchumi.Alieleza kuwa elimu hiyo inalenga kupunguza matumizi ya nishati zinazochangia uharibifu wa mazingira, sambamba na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya majiko ya umeme ambayo ni rahisi, salama na yenye ufanisi mkubwa katika kupikia.Kwa upande wake, Balozi Coppola alieleza kufurahishwa na namna TANESCO inavyoshirikiana na Serikali katika kusambaza huduma za umeme kwa wananchi, akibainisha upatikanaji wa nishati safi ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu, kulinda mazingira na kukuza uchumi wa jamii kwa ujumla.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment