" BULIGE FC YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA KWA PENATI DHIDI YA MANHEIGANA FC

BULIGE FC YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA KWA PENATI DHIDI YA MANHEIGANA FC

Na Mapuli Kitina Misalaba

Timu ya Bulige FC kutoka Wilaya ya Kahama imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa penati 4-1 dhidi ya Manheigana FC katika mchezo mkali uliochezwa leo Juni 11, 2026 kwenye Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida, huku timu zote zikishindwa kutumia nafasi walizozipata kutikisa nyavu.

Kutokana na sare hiyo, mshindi alitafutwa kwa mikwaju ya penati ambapo Bulige FC ilionesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kufunga penati nne dhidi ya moja ya Manheigana FC, matokeo yaliyoifanya kutinga hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha wa Bulige FC ameushukuru uongozi wa mashindano pamoja na mashabiki wao kwa ushirikiano waliouonesha, huku akiahidi kuwa timu hiyo itaendelea kupambana kwa bidii katika hatua zinazofuata za mashindano.

Kwa upande wake, kocha wa Manheigana FC amepongeza maandalizi ya mashindano hayo na kuushukuru uongozi wa NIACHEKONA CUP kwa kuwapa nafasi ya kushiriki, akieleza kuwa licha ya kuondolewa wamejifunza mambo mengi na watarejea wakiwa imara zaidi katika mashindano yajayo.

Katibu wa Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP, Sambayi Jilya, ametangaza kuwa mchezo wa kesho utawakutanisha Sangu FC na Kashishi FC katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikisaka nafasi ya kusonga mbele.

Sambayi Jilya amewahimiza wananchi na wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwabenda ili kushuhudia vipaji mbalimbali vya vijana vinavyoendelea kuoneshwa kupitia mashindano hayo.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo, kuimarisha mshikamano wa jamii na kudumisha amani.

Kwa mawasiliano ya shughuli mbalimbali za michezo, matangazo na ushereheshaji wa matukio, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Kikosi cha Manheigana FC.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post