
Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha .Mkuu wa wilaya ya Arusha Joseph MKude ameipongeza mamlaka ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya DCEA na Wadau mbalimbali Kwa kazi kubwa ya kusaidia waraibu na kutoa wito Kwa jamii kujenga upendo na ukaribu kwa watu wanaotumia dawa hizo kama njia muhimu ya kuwafanya waachane na matumizi hayo. Akizungumza katika maadhimisho ya kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya duniani, Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Arusha MKude amesema mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya si ya kutegemea mamlaka husika (DCEA) tu bali wadau na jamii nzima inatakiwa kuwajibika."Katika halmashauri yetu kuna fulsa ya mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Natoa wito Kwa vijana wote mnaopata matibabu, mkishapona undeni vikundi njooni ofisini kwangu nitawasaidia mpate mikopo muinue uchumi wenu"amesema MKude.Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii mamlaka ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya DCEA Kanda ya Kaskazini Brenda Mbati amesema Kwa mwaka mmoja 2025/2026 wamefanikiwa katika mkoa wa Arusha kufanya operesheni 121, na kukamata watuhumiwa 413, wanaume 338 na wanawake 75, dawa zilizokamatwa ni mirungi kilo 1458.26 na bangi kilo 2977.03.Aidha amesema katika Mkoa wa Kilimanjaro zimefanyika operesheni 50, na kukamata watuhumiwa 72 wanaume 50, na wanawake 22, dawa zilizokamatwa ni mirungi kilo 1568.61 na bangi kilo 13.02. Katika Mkoa wa Tanga zimefanyika operesheni 49 na kukamata watuhumiwa 33, wanaume 30, na wanawake 3, dawa zilizokamatwa ni mirungi kilo 1814.49, bangi kilo 20.25 na heroin gramu 14.Vilevile katika mkoa wa Manyara operesheni 7, watuhumiwa 32, wanaume 24 na wanawake 8, dawa zilizokamatwa ni mirungi kilo 575.90.Brenda amesema Kwa ujumla Kanda ya Kaskazini zimefanyika operesheni 227 na kukamata jumla ya watuhumiwa 550 wanaume 442 na wanawake 108, dawa zilizokamatwa katika mikoa yote minne ni mirungi kilo 5417.26, bangi kilo 3010.30 na heroin gramu 14.Katika namna hiyohiyo shuhuda aliyetumia dawa Kwa miaka 15 na badae kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Flora Manongi (39) amesema anamshukuru Mungu na wote waliohusika kumsaidia kuacha matumizi ya dawa za kulevya."Nilitumia vilevi vyote, nilifanyiwa vitendo vya ukatili, nilikuwa mwizi na mlevi kupitiliza, nilichoka sana, familia yangu ilinitenga lakini wakati ulipofika nilikubali kubadilika na kwenda katika nyumba za kusaidia waraibu(Sober House) na Sasa ni miaka 7 situmii kilevi chochote"amesema.Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mratibu wa afya ya akili wa Mat clinic hospitali ya Mount meru Arusha Magreth Msigwa amesema idadi ya Wateja waliojisajili kupata huduma hadi Sasa ni 907, waliohitimu baada ya kupona ni 130, waliopoteza maisha wakati wakitibiwa ni 33 na waliowezeshwa mitaji na kupelekwa shule 28."Tunaiomba serikali na Wadau wengine wa maendeleo kushirikiana nasi kuwawezesha wateja kiuchumi pindi wanapopona Ili kuhakikisha hawarudii tena kutumia dawa za kulevya. Wengi wao wamekuwa wakishindwa kuacha dawa kwa sababu ya kukosa shughuli ya kuwaingizia kipato" amesema Magreth.Vilevile Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mashitaka Nchini Filbert Msuya amesema ni wajibu wa kila mmoja katika jamii kuwaibua wauza dawa za kulevya Ili wafikishwe mahakamani na kupewa adhabu stahiki.Pia Shuhuda aliyeacha kutumia dawa za kulevya na mmiliki wa nyumba ya kusaidia wengine Beda Shirima, amewataka vijana wenzake kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na kuiomba serikali kutumia nguvu yake kuwakamata wote wanaohusika na uuzaji wa dawa hizo ili waadhibidhiwe vikali.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment