" ELECT ARUSHA YAZINDUA KAMBI YA MATIBABU BURE, WATAALAM WA JKCI WASHIRIKI

ELECT ARUSHA YAZINDUA KAMBI YA MATIBABU BURE, WATAALAM WA JKCI WASHIRIKI


Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media Wananchi wameanza kupatiwa matibabu bure kwenye kambi ya siku tatu katika chuo Cha Afya na sayansi shirikishi Arusha Lutheran (ELCT) kilichopo Halmashauri ya wilaya Arusha, Akifungua zoezi la utoaji huduma, Katibu Mkuu wa afya Dayosisi ya Kaskazini na Mkurugenzi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni Dkt. Amon Martin amesema licha ya Kanisa kutoa elimu, kuhubiri injili pia ina jukumu la kurejeza afya na afueni Kwa wagonjwa.Ametaja huduma zitakazotole kuwa ni pamoja na huduma macho, meno, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya wanawake huku akiwataka wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa ajili ya kupata huduma hizo kwani hutolewa bure."Lakini pia kutakuwa na huduma ya magonjwa kwa watoto pamoja na magonjwa ya moyo na tezi dume, hivyo kipekee nawapongeza na kuwashukuru Hospitali za AICC, Selian ya mjini na Ngaramtoni, Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na udhamini wa Kampuni ya utalii ya TANZANIA SPECIALIST. Naamini Kwa umoja wetu tutasaidia wananchi wengi"Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Arusha Lutheran (ELCT) Lilian Shuma amesema kambi ya madaktari itasaidia kutoa huduma ya afya Kwa watu wengi ambao hawana uwezo kifedha wa kupima afya zao, pia imekuwa fursa ya kutangaza chuo hicho Kwa muhula mpya wa masomo unaoenda kuanza.Amewakumbusha wananchi kutumia fursa hiyo kuwaona Madaktari Bingwa waliopo katika kambi ili kujua afya zao sambamba na hayo amewataka wazazi na walezi kuwaaandikisha watoto wao katika chuo hicho kinachotoa masomo ya afya na sayansi shirikishi.Amesema wanatarajia kupokea wagonjwa takriban  2500 kwa siku tatu ambazo matibabu yatafanyika."Chuo chetu kina miundombinu bora ya kujifunzia, hosteli za kutosha, chakula safi pia Kuna Hospitali za uhakika kufanyia mazoezi na kujifunza kwa vitendo" amesema Lilian.Mmoja wa wagonjwa anayesumbuliwa na matatizo ya macho Beatrice Mollel aliyefika kambini  hapo na kupatiwa matibabu, ameshukuru chuo na hospitali zote zilizojitolea Madaktari wake kuwahudumia wananchi." Nina Imani nitapona, nawaambia na wenzangu waje wapatiwe huduma hii bila malipo" Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka JKCI Seliani - Arusha Dkt.Advotus Kimogogoro amesema Kasi ya ongezeko la magonjwa ya moyo imekuwa kubwa kutokana na jamii kutokuwa na desturi ya kufanya mazoezi, kula chumvi nyingi, mfumo wa maisha na kutokula vyakula vya asili."Nashauri jamii iwe na utaratibu wa kupima afya na kutumia vyema kambi za matibabu pindi zinapokuwepo, na iwapo wataona dalili kama kuvimba miguu, kupumua Kwa shida hakikisha unamuona Daktari" amesema Dkt. Kimomogoro.Awali akifungua matibabu Kwa sala Mlezi wa Chuo Mchungaji Mariam Charity amesema Mungu anaponya lakini ni muhimu kutumia wataalamu wa afya waliowekwa na Mungu ili kusaidia kurejesha afya."Kila mmoja apende kukagua afya yake Kila wakati na sisi Watumishi wa Mungu tunaendelea kutimiza kusudi letu kama Mungu alivyotuagiza "(Luka 9:2).

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post