Na Mapuli
Kitina Misalaba
Bingwa
mtetezi wa NIACHEKONA CUP 2024, Sangu FC kutoka Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa
Mwanza, ameaga rasmi mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kufungwa kwa
mikwaju ya penati na Kashishi FC katika mchezo uliochezwa leo Juni 12, 2026 kwenye
Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa.
Mchezo huo
uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi ulimalizika kwa sare ya
bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida, huku Sangu FC ikishindwa kutumia
vyema nafasi ilizozipata ili kutafuta bao la ushindi.
Kutokana na
matokeo hayo, mshindi alitafutwa kwa mikwaju ya penati ambapo Kashishi FC
ilifanikiwa kupata penati nne dhidi ya tatu za Sangu FC na hivyo kuandika
historia ya kumuondoa bingwa mtetezi wa mashindano hayo.
Ushindi huo
wa Kashishi FC umeibua mshangao kwa mashabiki wengi wa soka, kwani timu hiyo
ilirejeshwa kwenye mashindano kupitia nafasi ya Best Rooza, huku wengi
wakiamini kuwa Sangu FC ilikuwa na nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake wa
mwaka 2024.
Akizungumza
baada ya mchezo huo, kocha wa Sangu FC kwa niaba ya timu yake amekubali matokeo
hayo na kuushukuru uongozi wa mashindano kwa nafasi waliyopewa kushiriki.
Aidha, amemuomba mwandaaji wa mashindano hayo kuendelea kuwapa fursa ya
kushiriki katika matoleo yajayo ya NIACHEKONA CUP.
Kwa upande
wao, viongozi wa Kashishi FC wameushukuru uongozi wa mashindano pamoja na
Kamati ya Mashindano kwa kuwaamini na kuwarudisha kwenye mashindano kupitia
nafasi ya Best Rooza. Wamesema ushindi dhidi ya bingwa mtetezi ni ishara kuwa
wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi na sasa wanaamini wanaweza kufika mbali na
hata kutwaa ubingwa wa mwaka huu.
Kwa matokeo
hayo, Sangu FC imehitimisha safari yake katika NIACHEKONA CUP 2026 huku
Kashishi FC ikitinga hatua ya robo fainali pamoja na timu nyingine zilizofuzu.
Mchezo huo pia umehitimisha rasmi hatua ya timu 12 bora na kufungua pazia la
hatua ya robo fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamati ya Mashindano, Makamu Mwenyekiti wa NIACHEKONA CUP, Samwel
Stephen, ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo Songambele Mhangu FC
kutoka Kata ya Salawe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga itamenyana na Ufukunyungu
FC kutoka Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga katika pambano la robo fainali
linalotarajiwa kuvutia mashabiki wengi.
Samwel
Stephen amewahimiza wananchi, wadau wa michezo na mashabiki kuendelea
kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwabenda ili kushuhudia michezo
mbalimbali inayoendelea kuibua vipaji vya vijana na kuimarisha mshikamano wa
jamii.
Mashindano
ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC
NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakiwa na lengo la
kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo, kuimarisha amani na mshikamano wa
jamii.
Kwa
mawasiliano ya shughuli mbalimbali za michezo, matangazo na ushereheshaji wa
matukio, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Sangu FC.
Wachezaji wa Sangu FC na Kashishi FC wakipambana kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya NIACHEKONA CUP 2026 katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki wengi.
Wachezaji wa Sangu FC na Kashishi FC wakipambana kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya NIACHEKONA CUP 2026 katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki wengi.
Ushindani mkubwa ukishuhudiwa Uwanja wa Mwabenda huku timu zote zikitafuta bao la ushindi ndani ya dakika 90 za mchezo.
Burudani ya soka ikiendelea kutawala katika NIACHEKONA CUP 2026 kupitia pambano kali kati ya Sangu FC na Kashishi FC.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa leo wa NIACHEKONA CUP 2026 katika Uwanja wa Mwabenda.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakishuhudia ushindani mkubwa wa timu zinazowania nafasi ya kusonga mbele katika NIACHEKONA CUP 2026.
Mashabiki wakifurahia burudani ya soka na ushindani mkubwa unaoendelea kushuhudiwa katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Mashabiki wakifurahia burudani ya soka na ushindani mkubwa unaoendelea kushuhudiwa katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa Sangu FC dhidi ya Kashishi FC katika Uwanja wa Mwabenda.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa Sangu FC dhidi ya Kashishi FC katika Uwanja wa Mwabenda.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





















Post a Comment