
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 imeziondoa
timu mbili kwenye mashindano hayo kutokana na ukiukwaji wa kanuni na taratibu
zilizowekwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Kamati ya Mashindano,
Makamu Mwenyekiti wa NIACHEKONA CUP, Bwana Samwel Stephen, amesema timu ya
Kimandaguli FC imeondolewa kwenye mashindano hayo kwa sababu za kinidhamu baada
ya baadhi ya mashabiki wake pamoja na benchi la ufundi kuhusika katika vitendo
vya fujo wakati wa mchezo.
Amesema pamoja na Kimandaguli FC kufanikiwa kufuzu na
kuingia hatua ya timu 12 bora, kamati imelazimika kuchukua hatua hiyo kwa lengo
la kulinda nidhamu, amani na heshima ya mashindano hayo.
Bwana Samwel Stephen amesema pia kuwa timu ya
Isenengeja FC kutoka Wilaya ya Misungwi imeondolewa kwenye mashindano hayo
baada ya kukiuka mara mbili kanuni za mashindano zinazohusu muda wa kufika
uwanjani.
Ameeleza kuwa mara ya kwanza kamati ilitoa onyo kwa timu hiyo baada ya kuchelewa kufika kwenye mchezo wake, lakini ilirudia kosa hilo kwa mara nyingine ambapo ilifika uwanjani majira ya saa kumi na moja jioni, jambo ambalo limeonekana kuhatarisha ratiba ya mashindano.
Makamu Mwenyekiti huyo amezitaka timu zote zilizosalia
kwenye mashindano hayo kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa ili kuhakikisha mashindano yanaendelea kwa amani, nidhamu na
ushindani wa haki.
Kwa mawasiliano ya huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha ISENENGEJA FC.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment