Baadhi ya mashabiki wa timu ya Home Boys FC kutoka
Kata ya Solwa wameonesha kujiamini kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ufukunyungu
FC kutoka Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, kwa kutabiri ushindi mnono wa timu
yao.
Wakizungumza na Misalaba Media, mashabiki hao wamesema
wana imani kubwa na kikosi cha Home Boys FC kutokana na kiwango kizuri
walichoonesha katika michezo iliyopita, huku baadhi yao wakitabiri timu hiyo
kuibuka na ushindi wa hadi magoli 10 dhidi ya wapinzani wao.
Wamesema wanaamini uwepo wa kocha mpya pamoja na
morali kubwa ya wachezaji utasaidia timu hiyo kufanya vizuri na kutinga hatua
inayofuata ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Hata hivyo, mashabiki hao wamewataka wachezaji wa Home
Boys FC kutobweteka na badala yake kuingia uwanjani kwa nidhamu, kujituma na
kupambana ili kutimiza matarajio ya mashabiki wao.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa
Mwabenda huku ukitarajiwa kuvutia mashabiki wengi kutoka Solwa, Ngokolo na
maeneo mengine ya Mkoa wa Shinyanga.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment