Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya MAWEMIRU FC imefanikiwa kutinga hatua
inayofuata ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuiondoa MAHEMBE FC
kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa
Mwabenda, kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika
kwa ushindi wa penati 4-2 kwa MAWEMIRU FC baada ya timu hizo kushindwa kupata
mshindi ndani ya dakika 90 za kawaida.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza, MAWEMIRU FC
ilifungwa bao 1-0 na MAHEMBE FC, hivyo kuingia uwanjani leo Mei 1, 2026 ikiwa
na jukumu la kusawazisha matokeo hayo ili kuendelea kusalia kwenye mashindano.
Katika dakika 90 za mchezo wa leo, MAWEMIRU FC
ilifanikiwa kupata bao moja muhimu lililofanya matokeo ya jumla ya michezo yote
miwili kuwa sare, hali iliyolazimu mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati kwa
mujibu wa kanuni za mashindano hayo.
Kwa ushindi huo, MAWEMIRU FC sasa itakutana na NYUNDO
FC katika hatua inayofuata ya mashindano hayo, baada ya NYUNDO FC kufuzu jana
kwa kuiondoa NZOZA FC kwa mikwaju ya penati.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Makamu Mwenyekiti wa
NIACHEKONA CUP, Bwana Samwel Stephen ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho
ambapo BAJAJI FC itamenyana na NYANDOLWA FC katika pambano linalotarajiwa kuwa
na ushindani mkubwa.
Ameendelea kuwahimiza wananchi, wadau wa michezo na
mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili kuendelea
kushuhudia vipaji vya vijana pamoja na burudani ya michezo inayotolewa kupitia
mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino (MC NIACHEKONA) kwa ufadhili wa shirika la Lushu Foundation yakiwa
na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo, kuimarisha amani na
kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa huduma za ushereheshaji wa matukio mbalimbali, matangazo na burudani, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Mawemiru FC
Wachezaji wa MAWEMIRU FC na MAHEMBE FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa marudiano leo Jumatatu Mei 1, 2026 katika ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda.
Wachezaji wa MAWEMIRU FC na MAHEMBE FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa marudiano leo Jumatatu Mei 1, 2026 katika ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda.
Wachezaji wa MAWEMIRU FC na MAHEMBE FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa marudiano leo Jumatatu Mei 1, 2026 katika ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment