MRADI wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Urejesho wa Mandhari ya Misitu nchini Tanzania (FOLUR), unatarajia kutoa mafunzo maalum kwa viongozi wa serikali za vijiji na shehia mbalimbali visiwani Zanzibar. Hatua hiyo inalenga kujenga uwezo wa kiutendaji na kuhakikisha jamii inatekeleza shughuli za mradi huo kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.Akifungua mafunzo hayo kwa maafisa ugani wa kilimo na misitu upande wa Zanzibar, Mratibu wa mradi huo, Bi. Miza Suleiman Khamis, alisema dhumuni kubwa ni kuwawezesha watendaji hao kubaini, kuepuka au kupunguza athari hasi zinazoweza kujitokeza kabla hazijaletea madhara wanajamii na mazingira yao.Kwa upande wake, Msimamizi wa Kitengo cha Jinsia, Usalama wa Mazingira na Jamii wa mradi huo, Bw. Revocatus Kadoshi, alibainisha kuwa viongozi wa shehia na maafisa ugani watafundishwa miongozo minne mikuu.Miongoni mwa miongozo hiyo ni Mpango wa Usimamizi wa Mazingira na Jamii (ESMP), unaohusu udhibiti wa matumizi ya rasilimali na kuzuia uhamishaji wa watu usio wa hiari.Bw. Kadoshi alifafanua kuwa mwongozo huo unalenga kudhibiti na kupunguza athari za kimazingira na kijamii wakati wa utekelezaji wa mradi. Aliongeza kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na matakwa ya Mwongozo wa Sera na Taratibu Jumuishi za Ulinzi wa Kijamii za Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF)."Viongozi hawa pia watafundishwa kuhusu Usimamizi Shirikishi wa Visumbufu. Huu unalenga kulinda afya na usalama wa jamii kwa kudhibiti athari zitokanazo na matumizi ya viuatilifu na mbolea," alisema Bw. Kadoshi.Aidha, mafunzo hayo yatahusisha mbinu za usimamizi wa mazingira zinazohakikisha ustawi wa jamii, usalama mahali pa kazi, pamoja na usafi wa mazingira wakati wote wa utekelezaji wa shughuli za mradi huo.Vilevile Aliongeza kuwa, ili kuhakikisha usalama wa jamii, mradi umeweka utaratibu maalumu wa kupokea nakufanyia kazi malalamiko kutoka kwa mwanajamii au kikundi cha kijamii kuhusiana na shughuli zinazotekelezwa na mradi. Hii inalwnga kuhakikisha jamii inashiriki vema kwenye shighuli za mradi na wanakuwa na nafasi ya kutoa dukuduku au lalamiko wakati wowote.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment