" MTENDAJI WA KATA YA SOLWA AWAHIMIZA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NIACHEKONA CUP

MTENDAJI WA KATA YA SOLWA AWAHIMIZA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NIACHEKONA CUP

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mtendaji wa Kata ya Solwa, Jackson Maganga, amewahimiza wananchi na mashabiki wanaofika uwanjani kuendelea kudumisha amani, utulivu na kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa ili mashindano hayo yaendelee kufanyika katika mazingira salama.

Maganga amempongeza mwandaaji wa mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, kwa kuandaa mashindano hayo ambayo amesema yamekuja wakati muafaka kwa wananchi wa kata hiyo.

Amesema kwa sasa wananchi wengi wa Solwa wanaendelea na shughuli za mavuno, hivyo amewahimiza kutumia muda wa asubuhi na mchana kufanya kazi za kilimo huku wakitumia nyakati za jioni kufuatilia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP yanayofanyika katika uwanja wa Mwabenda.

Amesema mashindano hayo yamekuwa sehemu ya burudani, mshikamano na kuwakutanisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali, huku yakitoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

Maganga amewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mashindano hayo, akieleza kuwa ina imani na jitihada zinazofanywa na MC NIACHEKONA katika kukuza michezo na kuhamasisha maendeleo ya vijana pamoja na jamii kwa ujumla.

Amewahimiza wananchi wa Solwa na maeneo jirani kuendelea kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo mbalimbali ya NIACHEKONA CUP 2026.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post