Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limemtia nguvuni Peter Willium (28), mkazi wa Kijiji cha Itale, Wilaya ya Chato kwa tuhuma za kumteka na kumbaka Mwanafunzi, ambaye utambulisho wake umehifadhiwa kwa mujibu wa sheria.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo la kusikitisha lilitokea tarehe 31 Mei 2026, majira ya saa sita mchana. Eneo la tukio ni Pori la Ichwankima lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Burigi, Wilaya ya Chato.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimvamia mwathirika, akamkokota hadi vichakani na kumfanyia ukatili wa kingono. Baada ya kitendo hicho, hakumuachia huru mwathirika. Badala yake, aliwasiliana na familia ya msichana huyo kupitia simu, akiwataka wamtumie fedha ili amwachie. Aliongeza vitisho kuwa atamdhuru iwapo hawataitikia matakwa yake.
Baada ya kupata taarifa, polisi walifanya operesheni ya kimsako na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa. Kwa sasa mahojiano yanaendelea na upelelezi unakaribia kukamilika ili mtuhumiwa afikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita amewashukuru wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo. Amehimiza jamii kuendelea kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto na wanafunzi. Pia ameonya kuwa jeshi hilo litachukua haytua kali kwa mtu yeyote atakayethibitika kuhusika na uhalifu wa aina yoyote.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment