Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akizindua maonesho ya mazingira katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026
Na Alex Sonna, Dodoma
SERIKALI imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika ubunifu wa teknolojia ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 1,2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mhe. Reuben Kwagilwa, wakati akifungua maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Amesema pamoja na changamoto hizo, Watanzania wameonyesha utayari mkubwa wa kushiriki katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia ubunifu wa teknolojia, matumizi ya sayansi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira.
Amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha usimamizi wa mazingira kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazosaidia kuongeza ufanisi katika uhifadhi wa rasilimali za asili na kukabiliana na changamoto za tabianchi.
“Nimepitia mabanda ya maonesho na kujionea ubunifu mkubwa unaofanywa na taasisi za serikali, sekta binafsi na vikundi vya wajasiriamali. Huu ni ushahidi kuwa Watanzania wako tayari kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mhe.KwagilwaAmesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 umeweka msisitizo mkubwa katika uhifadhi wa mazingira na kuongeza uwezo wa taifa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo amesema kuwa Tanzania inapoteza takribani hekta 370,000 za misitu kila mwaka, hali inayotishia juhudi za uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini.
Amesisitiza kuwa mafanikio ya juhudi za uhifadhi wa mazingira yanategemea ushirikiano wa wananchi, sekta binafsi na taasisi mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kulinda mazingira.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda, amesema maandalizi ya maonesho hayo yamekamilika na kwamba wananchi watapata fursa ya kujifunza kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kukabiliana nazo.
Amesema maonesho hayo yatahusisha wadau mbalimbali wa mazingira watakaowasilisha teknolojia, ubunifu na elimu itakayosaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutumia rasilimali za asili kwa njia endelevu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa Juni mosi, 2026 akiwasili katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma kufungua maonesho ya mazingira ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026. Anayempokea ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akikagua mabanda ya maonesho katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akizindua maonesho ya mazingira katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment