
Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya MAWEMIRU FC imefanikiwa kutinga hatua
inayofuata katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuiondoa NYUNDO FC
kwa ushindi wa penati 4-3 kwenye mchezo ambao umechezwa katika uwanja wa
Mwabenda, kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika
kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyolazimu mshindi
kupatikana kwa mikwaju ya penati kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo.
Katika kipindi cha kwanza, MAWEMIRU FC ilifanikiwa
kupata bao moja lililowapa matumaini ya kuendelea kutafuta ushindi. Hata hivyo,
NYUNDO FC walirejea kwa nguvu kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao
hilo, na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baada ya sare hiyo, timu hizo zilielekea katika hatua
ya mikwaju ya penati ambapo MAWEMIRU FC ilionesha umakini mkubwa na kufanikiwa
kushinda kwa penalti 4-3, ushindi uliowapa nafasi ya kusonga mbele huku
ukiihitimisha safari ya NYUNDO FC katika mashindano hayo ya mwaka 2026.
Viongozi na mashabiki wa NYUNDO FC wameishukuru Kamati
ya Mashindano pamoja na mwandaaji wa ligi hiyo kwa kuwapa nafasi ya kushiriki
mashindano hayo huku wakiahidi kurejea kwa nguvu zaidi katika mashindano
yajayo.
Akizungumza katibu wa Mashindano ya NIACHEKONA CUP, Sambayi
Jilya ametangaza ratiba ya mchezo unaotarajiwa kuchezwa kesho ambapo Duara FC
itamenyana na Songambele Mhangu FC katika pambano linalotarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu hizo katika mashindano
yanayoendelea.
Amewahimiza wananchi, wadau wa michezo na mashabiki wa
soka kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili kushuhudia burudani ya
soka pamoja na kuendelea kuunga mkono juhudi za kuibua vipaji vya vijana
kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na
Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa shirika la Lushu
Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha amani,
kukuza michezo na kuchochea maendeleo ya kijamii.
Kwa mawasiliano ya huduma za ushereheshaji wa shughuli
mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia
namba 0757 267 738.
NIACHEKONA CUP MWABENDA – WEKA TU WEKE.
MAWEMIRU FC na NYUNDO FC wakioneshana ushindani mkubwa katika pambano la kusaka tiketi ya hatua inayofuata ya NIACHEKONA CUP 2026.
MAWEMIRU FC na NYUNDO FC wakioneshana ushindani mkubwa katika pambano la kusaka tiketi ya hatua inayofuata ya NIACHEKONA CUP 2026.

Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia mchezo kati ya MAWEMIRU FC na NYUNDO FC.

Watangazaji wa mechi.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa makini pambano kali kati ya MAWEMIRU FC na NYUNDO FC.
Mchezo ukiendelea kwa kasi huku timu zote zikitafuta bao la ushindi mbele ya mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja wa Mwabenda.
Mchezo ukiendelea kwa kasi huku timu zote zikitafuta bao la ushindi mbele ya mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja wa Mwabenda.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment