" PROF. MBARAWA ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTABIRI WA HALI YA HEWA.

PROF. MBARAWA ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTABIRI WA HALI YA HEWA.

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia na vifaa vya kisasa katika kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa nchini.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya nne ya masuala ya hali ya hewa duniani inayofanyika Jijini Arusha, amesema matumizi ya mifumo ya kisasa yatasaidia kupata matokeo sahihi zaidi yanayoweza kusaidia maamuzi katika sekta mbalimbali za maendeleo.Aidha, ametoa shukrani Kwa shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) kufanya mkutano huo muhimu nchini Tanzania, akieleza kuwa ni mara ya kwanza kwa mkutano wa aina hiyo kufanyika katika Bara la Afrika na hususan Tanzania."Hatua hii inaonesha imani ya kimataifa kwa uwezo wa nchi katika kushiriki mijadala na maendeleo ya masuala ya hali ya hewa. Kupitia mkutano huu washiriki wataweza  kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi" Amesema Prof. Mbarawa.Pia amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya teknolojia yataimarisha uwezo wa nchi katika utabiri wa hali ya hewa, kutoa tahadhari mapema na kulinda maisha pamoja na mali za wananchi. Amesema  taarifa sahihi za hali ya hewa zitakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha sekta za kilimo, maji pamoja na shughuli za anga.Katika namna hiyo hiyo Naibu Katibu Mkuu wa shirika la hali ya hewa Duniani Dkt. Ko Barret amesema Jukwaa hili linategemewa kuwa la manufaa katika kujadili matumizi ya teknolojia  katika masuala ya utabiri wa Hali ya hewa Duniani." Kila mmoja ni shahidi kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi ni changamoto kubwa ulimwenguni ikiwemo mafuriko, vimbunga na kuongezeka Kwa joto duniani, sasa ni wakati sahihi kukaa pamoja na kuona jinsi tutaweza kurithisha kizazi kijacho  dunia ambayo imejipanga kukabili mabadilko haya" Amesema Dkt. Ko.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini Ladislaus Chan'ga amefafanua kuwa, Warsha hiyo imewaleta pamoja wataalam na wabobezi wa masuala ya hali ya hewa takriban 200 kutoka Duniani kote, lengo ni kutaka kuimarisha ufanisi wa utabiri wa hali ya hewa na ukusanyaji wa taarifa Kwa lengo la tahadhari za mapema.Pia Chan'ga amesema mamalaka ya Hali ya hewa nchini wamepiga hatua kubwa katika kuimarisha utabiri wa Hali ya hewa ambao Kwa asilimia 80% unatoa matokeo ya kweli."Natoa wito Kwa wananchi waendelee kuzingatia taarifa zinazotelewa na mamlaka ya Hali hewa nchini (TMA) ili kulinda Mali zao na kuepuka maafa" Amesema.Hata hivyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Afrika ametilia mkazo kizazi kipya (vijana) kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia nchini."Teknolojia inakua kasi,  kila mmoja ni shahidi kuwa bila kuendana na mabadiliko haya hatuwezi kukua kiuchumi Wala Kufikia malengo makubwa kama dunia inavyotutaka tuwe" Amesema Dkt. Kijazi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post