Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya Ufukunyungu FC kutoka Kata ya Ngokolo, mjini
Shinyanga imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika mashindano ya NIACHEKONA
CUP 2026 baada ya kuiondoa Home Boys FC ya Kata ya Solwa kwa ushindi wa penati
4-3.
Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki
wengi ulimalizika kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida,
huku timu zote zikishindwa kutumia nafasi walizozipata kutikisa nyavu.
Kutokana na sare hiyo, mshindi alitafutwa kwa mikwaju
ya penati ambapo Ufukunyungu FC ilionesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kupata
penati nne dhidi ya tatu za Home Boys FC.
Ushindi huo umeifanya Ufukunyungu FC kusonga mbele
katika hatua inayofuata ya mashindano hayo huku ukiihitimisha safari ya Home
Boys FC, timu ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa na mashabiki wengi wa Solwa
kufika mbali katika mashindano hayo.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya
Mashindano ya NIACHEKONA CUP, Sambayi Jilya, ametangaza ratiba ya mchezo wa
kesho ambapo Nyandolwa FC itamenyana na Shilabela FC katika pambano
linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikisaka nafasi ya
kusonga mbele.
Sambayi Jilya amewahimiza wananchi, wadau wa michezo
na mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwabenda ili
kushuhudia michezo mbalimbali inayoendelea kuibua vipaji vya vijana kupitia
mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana
Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu
Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo,
kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kuendelea kudumisha amani kupitia
michezo.
Kwa mawasiliano ya shughuli mbalimbali za kijamii,
michezo, matangazo na ushereheshaji wa matukio, wasiliana na MC NIACHEKONA
kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Ufukunyungu FC
Kikosi cha Home Boys FC.
Wachezaji wa Home Boys FC na Ufukunyungu FC wakioneshana ushindani mkubwa katika pambano la kusaka tiketi ya hatua inayofuata ya NIACHEKONA CUP 2026.
Wachezaji wa Home Boys FC na Ufukunyungu FC wakioneshana ushindani mkubwa katika pambano la kusaka tiketi ya hatua inayofuata ya NIACHEKONA CUP 2026.
Wachezaji wakionesha kiwango cha hali ya juu leo Juni 9, 2026 katika mashindano ya NIACHEKONA CUP yanayoendelea kuvutia mashabiki wengi.
Wachezaji wakionesha kiwango cha hali ya juu leo Juni 9, 2026 katika mashindano ya NIACHEKONA CUP yanayoendelea kuvutia mashabiki wengi.
Diwani wa Kata ya Solwa pamoja na Diwani wa Kata ya Mwakitolyo wakiwa miongoni mwa viongozi waliojitokeza kufuatilia mchezo wa leo wa NIACHEKONA CUP 2026.
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu pambano la Home Boys FC dhidi ya Ufukunyungu FC katika Uwanja wa Mwabenda.
Wachezaji wakionesha kiwango cha hali ya juu leo Juni 9, 2026 katika mashindano ya NIACHEKONA CUP yanayoendelea kuvutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo wa leo Juni 9, 2026 katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 katika Uwanja wa Mwabenda.

Wananchi wa Solwa, Ngokolo na maeneo jirani wakifurahia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Wananchi wa Solwa, Ngokolo na maeneo jirani wakifurahia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment