Wananchi wa kata ya Mkululu na maneno jirani wilayani Masasi mkoani Mtwara wameanza kunufaika na huduma bora za usafiri na usafirishaji kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika barabara ya Chingutwa–Songambele.
Ujenzi huo uliotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE programu ya uondoaji vikwazo vya barabara (Botleneck) umekuwa na manufaa makubwa hasa urahisi wa usafirishaji wa mazao ya wakulima.
Meneja wa TARURA wilaya ya Masasi, Mhandisi John Kimario amesema changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wananchi ni usafirishaji wa mazao ya mashambani kwa sababu katika wilaya hiyo wananchi wanategemea kilimo cha korosho, ufuta na mbaazi.
”Mfumo wa uuzaji wa mazao ni kupitia maghala kwa maana yanapitishwa ghalani halafu yanasafirishwa kwenda maeneo mengine. Kabla ya ujenzi wa daraja hili usafirishaji wa mazao haya kutoka mashambani kwenda kwenye maghala ilikuwa ni changamoto kubwa”, amesema Mhandisi Kimario.
Amesema baada ya ujenzi wa daraja hilo kwa sasa magari yote yanapita na mizigo ikishapokelewa ghalani inasafirishwa kwa urahisi kwenda katika maeneo yaliyokusudiwa na kuongeza kuwa wananchi wa maeneo hayo wamefurahishwa sana mradi huo kwa sababu unaunganisha kata tatu za Mkululu, Chingutwa na Lulindi.
Kwa upande wake, Khalid Masinde ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Makululu amesema kabla ya ujenzi wa daraja hilo kipindi cha masika mvua zikinyesha walikuwa wakisubiri kwa muda mrefu kuvuka wakati wa kwenda shule hivyo kuchelewa kufika kwa wakati.
Naye, Latifa Rajabu mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Mkululu amesema kipindi cha masika mvua zikinyesha walikuwa wanasubiri mpaka zikatike ndo wavuke kwenda shule lakini kwa sasa baada ya ujenzi wa daraja wanapita vizuri hata mvua ikinyesha.
Vile vile, Habibu Abdallah mkazi wa Mkululu amesema kabla ya ujenzi wa daraja walikuwa wanapata shida kubwa ya usafirishaji hasa kipindi cha mwezi Desemba ambapo mvua huwa nyingi katika eneo hilo.
”Kwa mfano mimi mwenyewe ni bodaboda nilikuwa napata tabu nikifika hapa na abiria inatubidi tusubiri masaa mawili hadi matatu na wakati mwingine hata siku mbili mvua zikichanganya lakini kwa sasa tunashukuru serikali wameturahisishia”, ameongeza Bw. Habibu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment