Timu ya Afya ya Akili na Msaada wa Kisaikolojia (MHPSS Team) ya Halmashauri ya Mji Kasulu imeridhia kuendelea kutoa elimu kuhusu afya ya akili kupitia makanisa, misikiti, shule na vyombo vya habari ili kuongeza uelewa wa jamii na kupunguza matukio ya ukatili.Mapendekezo hayo yametolewa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri hiyo ambapo timu hiyo imejadili masuala mbalimbali ikiwemo afya ya akili, magonjwa ya mlipuko na matukio ya ukatili katika jamii.Akitoa elimu kuhusu afya ya akili, Mratibu wa Magonjwa ya Afya ya Akili wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Augustin Karol amesisitiza umuhimu wa kutambua dalili mapema na kuwahi kupata huduma za kitaalamu ili kudhibiti athari za matatizo ya afya ya akili.Kwa upande wake, Mratibu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya mlipuko Benjamin Machonko amesema Halmashauri imeimarisha inaendelea kufuatilia kwa ukaribu magonjwa ya mlipuko na kuandaa mpango wa dharura wa kuimarisha utayari wa vituo vya afya na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kinga dhidi ya Ebola.Katika hatua nyingine, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo, Salum Masagha amesisitiza umuhimu wa malezi na makuzi bora kwa watoto na kuwahimiza wananchi kutoa taarifa za ukatili mapema ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment