
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido, akipokea Tuzo ya Rais ya Mlipakodi Kinara kwa niaba ya Barrick Mining Corporation kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi Wakubwa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido (wa nne kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni mengine yanayolipa kodi kubwa serikalini, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi Wakubwa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
****
Kampuni ya madini ya Barrick Mining Corporation yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation imeendelea kushikilia rekodi ya kulipa kodi kubwa kwa Serikali ambapo imetangazwa na kutunukiwa tuzo ya Rais ya Mlipa kodi mkubwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Tuzo hiyo imetangazwa na kutolewa wakati wa hafla Siku ya kutoa tuzo tuzo kwa walipa kodi wakubwa iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika Hafla hiyo Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza makampuni na taasisi ambazo zimekuwa zikilipa kodi kwa uaminifu na kuwezesha Serikali kupata fedha za kuimarisha uchumi wa nchi na kufanikisha kutekeleza miradi ya maendeleo ya kuwezesha maisha na ustawi wa wananchi kuwa bora zaidi.
Tuzo hii kwa Barrick ni mwendelezo wa kutambuliwa mchango wake katika kuchangia pato la taifa kwa njia ya kodi ambapo katika miaka iliyopita pia imeshinda hii na kutambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania miongoni mwa makampuni yanayoongoza kulipa Kodi kubwa nchini.
Mbali na kupata tuzo hii ya kodi, Barrick-Twiga mwaka huu pia imekuwa kinara wa kutoa gawio kwa serikali ambapo imetoa kiasi cha shilingi bilioni 221.9 .
Migodi inayoendeshwa chini ya ubia wa Barrick na Twiga Minerals nchini ni North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, ambao upo katika mchakato wa kufungwa na kwa sasa umegeuzwa kuwa Kongani Maalum ya Kimataifa ya Sekta ya Madini inayojulikana kama Buzwagi Economic Special Zone.
Barrick pia imekuwa ikichangia Pato la Serikali kupitia malipo, gawio, mrabaha, tozo mbalimbali na mdau mkubwa wa kuchangia uchumi wa kijamii kupitia mtandao wa biashara zake.
Akiongelea mafanikio haya kwa kampuni kuendelea kufanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo nchini, Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido amesema utekelezaji wa mikakati endelevu ya kampuni na ubia wake na Serikali unaendelea kuleta matokeo bora na kufanikisha wananchi kunufaika na Raslimali za madini.
Barrick pia imekuwa ikitekeleza sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa ufanisi ambapo kwa kiasi kikubwa imefanikisha kutekeleza miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi yake hususani katika sekta za elimu, afya, maji safi na salama pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment