" CHONGOLO APONGEZA MAENDELEO WILAYANI ARUMERU

CHONGOLO APONGEZA MAENDELEO WILAYANI ARUMERU


*Ashauri Wananchi Wilayani humo Kuwekeza katika Utalii wa Asili*Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arumeru-Arusha.Waziri wa kilimo na  Mlezi wa Mkoa wa Arusha Daniel Chongolo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi Wilaya ya Arumeru amepongeza kasi kubwa ya maendeleo katika sekta ya kilimo, miundombinu ya barabara, elimu, afya na huduma nyingine nyingi.Amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo nchini, na itahakikisha upatikanaji wa masoko, miundombinu ya barabara, huduma za ugani na uhakika wa pembejeo Ili wakulima  waweze kunufaika.Aidha amewataka wananchi Wilayani humo kuwekeza katika Utalii wa Asili Ili wajiingizie fedha nyingi za kigeni. Ametoa mfano wa Jamii ya Wamasai ambao tayari wamewekeza na wanavuna takribani Billions 2 kila mwaka.Vilevile Chongolo amewataka viongozi kusimamia vyema miundombinu yamaji inayojengwa. Amesema atazungumza na Waziri wa Maji Jumaa Aweso ili asukume fedha kwenye mamlaka ya maji au Wakala wa Maji Vijijini lengo ni kuona kilimo kinatekelezwa bila vikwazo."Wananchi tunzeni amani na utulivu wa nchi, hatuna nchi nyingine ya kwenda, ila hii tu. Tufanye kazi na kuhamasisha amani, serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo lengo ni kuona kila Mtanzania anaishi maisha bora"Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameiomba serikali kuboresha mazingira ya wakulima ili kuongeza tija na kuinua uzalishaji wa mazao kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa Taifa.Nassari akizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Waziri wa Kilimo, amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani kwenda sokoni na kupunguza gharama kwa wakulima."Kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo Arumeru mashariki Kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, serikali ihakikishe upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, kuimarisha huduma za ugani na kuwapatia wakulima masoko ya uhakika yatakayowawezesha kuuza mazao yao kwa bei yenye tija"Pia, Nassari amesisitiza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika shughuli za kilimo pamoja na kulinda maeneo ya kilimo yasivamiwe au kuingiliwa na shughuli nyingine za maendeleo, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji na kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post