" DIWANI WA RUZINGA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU.

DIWANI WA RUZINGA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU.

 



Na Avitus Benedicto, Missenyi

Diwani wa Kata ya Ruzinga, Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, Mhe. Aspon Mwijage, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia uboreshaji wa miundombinu ya shule.

Mhe. Aspon ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ruhija.

Amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi Milioni 24 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika Kata ya Ruzinga, hatua ambayo itaongeza ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Amesema kuwa Serikali imetoa shilingi milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Ruhija, mradi unaotarajiwa kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na kuboresha huduma za elimu kwa wanafunzi.

Aidha, Mhe. Aspon amewahimiza Wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo. 

Katika mkutano huo, Wananchi wa Kijiji cha Ruhija  walikubaliana kwenye kaya moja hata wakiwa watu  10 kila mmoja atachangia kiasi Cha shilingi elfu tano kwa mwenye uwezo wa kufanya kazi na kuanzia miaka 18 kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo ya kata, huku vijana wenye uwezo wa kufanya kazi wakihamasishwa kushiriki kikamilifu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Aspon ameahidi kutoa zaidi ya shilingi Milioni moja kama motisha kwa vitongoji vya Kijiji cha Ruhija vitakavyofanya vizuri katika utunzaji wa mazingira na kuchangia maendeleo ya kata.

Amesema lengo ni kuhamasisha ushindani chanya, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Akihitimisha, Mhe. Aspon amesema maendeleo ya elimu na sekta nyingine za kijamii yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na Wananchi, akisisitiza kuwa ushiriki wa jamii katika miradi ya maendeleo ni nguzo muhimu ya kuijenga Ruzinga yenye maendeleo endelevu.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post