Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema madai kuwa amevunja Katiba kwa kuelekeza kusitishwa kwa mikutano ya hadhara hayana msingi, akisisitiza kuwa agizo hilo lilitolewa kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi zinazohusu mikusanyiko na maandamano.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katambi alisema waandaaji wa maandamano au mikutano ya hadhara wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya husika angalau saa 48 kabla ya tukio, wakieleza mahali, muda na madhumuni ya mkusanyiko huo. Alieleza kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kusimamisha mkusanyiko iwapo utahatarisha usalama, amani au maslahi ya umma.
Kauli hiyo imekuja kufuatia ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, wanasheria na wanaharakati waliodai kuwa alivunja Katiba baada ya kutoa agizo la Julai 26, 2026 akiwa Bungeni jijini Dodoma, ambapo alimwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camilius Wambura, kusitisha utoaji wa vibali vya mikutano ya hadhara.
Katambi alisema agizo hilo lililenga kuimarisha usalama wa nchi na kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza kutokana na tishio la kiusalama ambalo Serikali imebaini, akisisitiza kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa maslahi ya umma na kwa mujibu wa sheria.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment