Familia ya Ndugu Bahati Alphonce Mkama kutoka Mkoa wa Geita inatoa taarifa ya kumtafuta kijana wao, Bahati Alphonce Mkama, ambaye alikuwa akifanya kazi ya bodaboda katika eneo la Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam.
Bahati alipotea tangu mwezi Julai, 2026, na hadi sasa amekuwa haonekani kwa zaidi ya wiki mbili. Wakati anapotea alikuwa na pikipiki aina ya Boxer yenye namba ya usajili MC 155 EXL.
Familia inaomba mtu yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kufahamu alipo au kumpata awasiliane na Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu, au apige simu kupitia namba:
📞 0744 473 662
Tafadhali shiriki taarifa hii ili kumsaidia kurejea salama kwa familia yake.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment