" MAKONDA AAHIDI MATIBABU KWA WAGONGWA WALIOPEWA RUFAA.

MAKONDA AAHIDI MATIBABU KWA WAGONGWA WALIOPEWA RUFAA.


 Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

Waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo na Mbunge wa Arusha Paul Makonda amesema atahakikisha  wagonjwa 258 waliopewa rufaa ya kwenda kufanyiwa upasuaji, wanapata matibabu bure bila kulipia kwa sababu ya hali zao duni.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Arusha Makonda amesema katika kambi ya matibabu iliyofanyika wiki iliyopita, jumla ya wananchi 24871 wamefanyiwa uchunguzi, kupata vipimo na matibabu

Aidha ameshauri wananchi kuchangamkia kupima afya zao kila inapopatikana fulsa ya kambi ya matibabu Ili kuchunguza afya zao kabla ya hali haijawa mbaya.

"Katika Kambi hii wagonjwa waliopima shinikizo la damu 6030 na Kati yao 1930  wamekutwa na shinikizo la juu la damu. Ni muhimu kuchunguza afya mara kwa mara Kwa sababu hawa wasingepima pengine wangekutwa na hali ngumu inayoweza kupelekwa kifo" .

Hata hivyo amesema kuwa magonjwa yote yalichunguzwa na ametoa wito Kwa wanaume hususan wenye umri mkubwa kujitokeza kuchunguza tezi dume mapema kwani  inatibika.

Makonda amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kuhakikisha vifaa tiba na vitendanishi vinakuwepo vya kutosha katika vituo vya afya na hospitali zote nchini.


Vile vile amewashukuru Madaktari bingwa, Madaktari wabobezi na wauguzi wote kutoka Hospitali ya taifa Muhimbili na hospitali zingine waliofanikisha kukamilika kwa matibabu hayo, na kutoa maelekezo dawa zote za thamani zaidi ya milioni 80 zilizobaki kupelekwa katika vituo vyote vya afya Jijini Arusha kusaidia wagonjwa.

Pia ametoa wito kwa wadau na watu wenye mapenzi mema kuendelea kujitoa kuchangia matibabu Kwa watu wasiojiweza. Amesema watu wema tayari wametoa zaidi ya milioni 200 zitakazosaidia katika kambi ya matibabu ijayo.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya Arusha Dk.Nindwa Maduhu amesema "Mimi na Kamati kuu tunaahidi kutekeleza agizo la Waziri Makonda kuhakikisha wagonjwa wote waliopewa rufaa, wanafanyiwa operesheni kama inavyotakiwa, na dawa tulizopokea tutazigawa katika vituo vya afya kama taratibu zinavyotutaka".

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254.

Post a Comment

Previous Post Next Post