
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu Dk. Alex Malasusa, amewahimiza waumini kulipa kodi kwa furaha kwa kuwa ndiyo inayoendesha nchi.
Akihubiri katika ibada maalumu ya uzinduzi wa Usharika wa Kibada ulioko wilayani Temeke, Dk. Malasusa Dk Malasusa alisema kodi si jambo linalofurahisha na halijaanza leo.
Katika hotuba yake, alisimulia pia kukutana kwake na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kodi (TRA) nchini Uingereza na kufurahishwa na jinsi wanavyojitahidi kuvuka malengo bila watu kupigwa pingu.
“Juzi nilipata neema, nilikuwa katika maadhimisho nikaalikwa kule Uingereza, nimerudi juzi tu na nikiwa huko nikakutana na Kamishna Mkuu wa TRA (Mamlaka ya Kodi) tukazungumza na alinifurahisha kwa jinsi ambavyo anajitahidi, watu watoe kodi kwa hiari.
"Nikamshukuru kwamba ninashangaa sisikii sana watu wanapigwa pingu lakini nasikia kila baada ya miezi kadhaa mmevuka lengo,” alisema akisisitiza kuwa kodi ndiyo inayoendesha nchi.
Aliendelea: “Nikamwambia (kamishna) uwe na hakika nitaanza kuwakumbusha washarika wawe wanalipa kodi. Jamani lipeni kodi, tena kwa furaha kwa sababu ndiyo inayotuendesha”.
“Nataka kuwakumbusha kwamba kodi ililipwa hata na Yesu mwenyewe, wewe ni nani? Kwa hiyo kodi ndiyo isipokuwa wao wana bahati kubwa sana kwamba watu ni waaminifu kulipa kodi na watu ni waaminifu kutunza fedha zinazokusanywa,” alisema.
Aidha, Askofu Malasusa aliwakumbusha wanaume kuepuka kuwa wagumu wa kutubu kwa Mungu na kwa watu wanaowazunguka, wakiwemo wake zao, akisisitiza kuwa toba inabadilisha tabia na kujenga mahusiano mema.
Akizungumzia historia ya usharika huo, ilielezwa kuwa ulianza na familia tisa pekee zilizofanyia ibada katika kibanda cha miti na makuti kabla ya kujenga jengo la matofali, na kwa sasa usharika huo umekua na una jumla ya waumini 1,200.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment