
SIMBA SC imepata ushindi kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya fainali ikipata ushindi mbele ya mpinzani wake mkubwa Azam FC.
Bao la ushindi limefungwa na Yahya Zayd kiungo wa Azam FC ambaye alijifunga dakika ya 62 wakati akipambana kuokoa faulo iliyopigwa na kiungo Ellie Mpanzu.
Hili linakuwa taji la nne kwa Simba SC ikirejea bara na ushindi ikitwaa taji ambalo lilikuwa mikononi mwa Yanga SC waliofungashiwa virago na Azam FC.
Msimu wa 2025/26, Simba SC vs Azam FC zimekutana mara 3 ambapo kila timu imepata ushindi mara moja, Azam FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika ligi na Simba SC imepata ushindi kwenye mchezo wa fainali.
Mchezo mmoja wa mzunguko wa pili kwenye ligi walitoshana nguvu wakigawana pointi mojamoja ndani ya dakika 90.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment