" MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI BILIONS 3 KUZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU

MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI BILIONS 3 KUZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika Halmashauri ya Wilaya Arusha kesho 2026, 09 ambapo utakagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi na kufanya uzinduzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph MKude amesema katika shamrashamra za kuukaribisha Mwenge wananchi wajitokeze kwa wingi kuupokea na kusikiliza jumbe mbalimbali zilizobebwa zinazohimiza amani na usalama wa taifa, mapambano dhidi ya rushwa na dawa za kulevya.

Joseph Modestus Mkude - DC Wilaya ya Arusha

"Mwenge utawasili majira ya saa moja na nusu asubuhi katika viwanja vya Magereza-Kisongo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla, Wakati huo Mwenge utakuwa ukitokea Wilaya ya Longido" amesema Mkude.

Hata hivyo ametaja miradi 7 itakayokaguliwa  katika Kata 7 na Tarafa 3 yenye thamani zaidi ya shilingi Billions 3 mradi wa maji tanki la ujazo lita 50,000 uliopo Kata ya Kimindorosi, ujenzi wa shule ya ghorofa Murieti, jengo la upasuaji Kata ya Moivaro, mradi wa chakula wa vijana Njiro na mradi wa nishati safi katika shule ya sekondari Arusha.

Vilevile ameitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na mradi wa Kuku wa Mayai na mradi wa ujenzi wa barabara ya Giriki uliopo Kata ya Sakina. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1.1 itakuwa kiunganishi cha mawasiliano ya barabara ya Moshi, Arusha na Longido.

Mwenge wa Uhuru Umebeba Kaulimbiu"Wote Tanzania ni Yetu Tushikamane Kwa Pamoja Kwa Ajili ya Maendeleo Yetu".

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post