Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha, ameongoza matembezi ya pamoja yaliyowashirikisha askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, wanachama wa Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center pamoja na Suma JKT ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Polisi Jamii yatakayofanyika Agosti 25, 2026.Akizungumza na washiriki mara baada ya matembezi hayo, ACP Tesha amesema shughuli hiyo imelenga kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii. Amesisitiza kuwa mafanikio ya dhana ya Polisi Jamii yanategemea ushiriki wa wananchi katika kuzuia na kupambana na uhalifu, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vinavyohatarisha usalama.Aidha, amewapongeza washiriki wote kwa kujitokeza kwa wingi na kuwataka kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazoandaliwa kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Polisi Jamii, akieleza kuwa ushirikiano kati ya polisi na jamii ni msingi muhimu wa kudumisha amani, usalama na maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment