" PLANT YA UCHENJUAJI DHAHABU NYANG'HWALE YAJIVUNIA USALAMA, AJIRA NA KUCHOCHEA MAENDELEO

PLANT YA UCHENJUAJI DHAHABU NYANG'HWALE YAJIVUNIA USALAMA, AJIRA NA KUCHOCHEA MAENDELEO

Na Paul Kayanda, Nyang'hwaleMENEJA wa moja ya mitambo ya uchenjuaji wa dhahabu (Gold Processing Plant) iliyopo Wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita, Kelvin Shoo, amesema kampuni hiyo imeendelea kuzingatia viwango vya usalama kazini, kutoa ajira kwa wananchi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii inayowazunguka.Shoo alisema plant hiyo ina jumla ya matanki manne, yakiwemo matanki sita yenye uwezo wa kubeba tani 30 na mengine sita yenye uwezo wa tani 40, hali inayowezesha shughuli za uchenjuaji kufanyika kwa ufanisi na kuongeza uzalishaji.Alisema kwa sasa kampuni imeajiri wafanyakazi 17 wa kudumu, huku ikitoa wastani wa ajira nane za kila siku kwa wananchi wanaoshiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji na huduma zinazohusiana na plant hiyo.Akizungumzia suala la usalama, Shoo alisema kampuni imeweka kipaumbele kikubwa katika kulinda afya za wafanyakazi na wananchi wanaoishi jirani na eneo la mradi huo."Hatua zote za usalama hufuatwa kabla ya kuanza kazi. Maji yenye kemikali yanadhibitiwa kwa kuhifadhiwa kwenye mashimo maalumu ili yasitoke nje ya eneo la plant na kuathiri wananchi wa Kijiji cha Mwamakiliga pamoja na mazingira," alisema.Aliongeza kuwa kampuni itaendelea kushirikiana na Serikali na wananchi katika kuchangia maendeleo ya kijamii, ikiwemo kuboresha sekta za afya, elimu na miundombinu ya barabara kwa kufanya matengenezo mara kwa mara ili kurahisisha shughuli za kiuchumi na usafirishaji.Hata hivyo, Shoo alisema changamoto kubwa inayowakabili ni uwepo wa makazi ya wananchi karibu na eneo la shughuli za uchenjuaji, jambo ambalo linaweza kuleta changamoto za kiusalama na upanuzi wa uwekezaji.Aliiomba Serikali kutenga eneo maalumu kwa ajili ya shughuli za uchenjuaji wa madini au kutafuta eneo mbadala la makazi kwa baadhi ya wananchi ili kutoa nafasi kwa uwekezaji kuendelea kwa usalama na ufanisi zaidi.Aidha, alisema tayari wameanza mazungumzo na baadhi ya wananchi ili kufikia mwafaka utakaowezesha shughuli za uwekezaji kuendelea huku haki na maslahi ya pande zote yakizingatiwa.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post