July 25, 2026 | 1:59 pm

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanya matendo ya huruma kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika kituo cha afya Ilembo kilichopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Akikabidhi msaada huo Julai 25, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kama sehemu ya jamii limeona ni vyema kufanya matendo ya huruma na kutoa faraja kwa wagonjwa hao ili wasijione wapweke.
Msaada uliotolewa kwa wagonjwa hao ni pamoja na taulo za kina mama, pempasi, sabuni, sukari, unga, mafuta ya kupaka, maji, juice, mafuta ya kupikia, miswaki na dawa za meno pamoja na kuchangia damu.
Akipokea msaada huo Mganga Mfawidhi kituo cha afya Ilembo Dr. Veneranda Musati amelishukuru Jeshi la Polisi kwa msaada huo na kutoa wito kwa jamii kuiga mfano huo kwa kuwa na moyo wa kusaidia wahitaji.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment