Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, ameagiza halmashauri zote za mkoa huo, kutopokea dawa za matumizi ya binadamu zenye muda wa matumizi uliobaki chini ya miezi 12, hatua inayolenga kulinda matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Ametoa agizo hilo leo julai 6,2026, wakati wa Baraza Maalum la kupitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), katika Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Amesema "Ndani ya mkoa huu wa Shinyanga, hatutakubali kabisa kuletewa dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu ambazo zimebakiza muda wa matumizi wa chini ya miezi 12.”
Amesema dawa zinaposambazwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati kisha kuisha muda wake wa matumizi, wananchi wanaanza kuilaumu serikali wakidhani dawa zimefichwa, ilhali tayari zilikuwa zimefikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma.
Aidha Mhita amewataka viongozi wa sekta ya afya mkoani humo, kuimarisha ukaguzi wa dawa zinazoingia katika maghala na vituo vya kutolea huduma ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya muda wa matumizi kabla ya kupokelewa.
Mwisho.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment