
Picha ya mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony inayotoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa za tiba mionzi. Serikali imeifunga mashine hiyo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ili kuboresha ubora, usahihi na ufanisi wa huduma za matibabu ya saratani nchini mradi uliogharimu shilingi bilioni 8.3.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Computech Healthcare Solutions, Hanif Popat wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia utendaji kazi wa mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony. Mashine hiyo iliyofungwa na Kampuni ya Computech Healthcare Solutions inatoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Computech Healthcare Solutions Hanif Popat na wafanyazi wa kampuni hiyo wakati wa ziara yao katika taasisi hiyo kwaajili ya kukagua mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony inayotoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Mark Mseti akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Computech Healthcare Solutions Hanif Popat wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia utendaji kazi wa mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony. Mashine hiyo iliyofungwa na Kampuni ya Computech Healthcare Solutions inatoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa.Picha ya mashine ya tiba mionzi ya ELEKTA Harmony inayotoa huduma za matibabu ya saratani kwa kiwango cha kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa za tiba mionzi. Serikali imeifunga mashine hiyo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ili kuboresha ubora, usahihi na ufanisi wa huduma za matibabu ya saratani nchini mradi uliogharimu shilingi bilioni 8.3.
Picha na ORCI
**************************************
Mashine ya Elekta Harmony inatumia teknolojia za kisasa za Image Guided Radiotherapy (IGRT) zinazowezesha utoaji wa tiba ya mionzi kwa usahihi wa hali ya juu kwa kuzingatia eneo halisi la uvimbe. Mashine hii hutumia mfumo wa kisasa wa kupanga na kutoa dozi ya mionzi kulingana na umbo na ukubwa wa uvimbe hivyo kulinda kwa kiwango kikubwa tishu na viungo vyenye afya vilivyo karibu na eneo linalotibiwa.
Mashine hii ina uwezo wa kutibu aina mbalimbali za saratani kwa kutumia mbinu za kibingwa na ubingwa bobezi, ikiwemo Volumetric Modulated Arc Therapy (VMAT), Intensity Modulated Radiotherapy (IMRT) na mbinu nyingine za kisasa zinazowezesha tiba kutolewa kwa usahihi mkubwa.
Kutokana na teknolojia yake ya hali ya juu, Elekta Harmony hupunguza muda ambao mgonjwa hutumia ndani ya chumba cha matibabu jambo linaloongeza faraja na utulivu wakati wa matibabu huku likiboresha ufanisi wa huduma na kuongeza idadi ya wagonjwa wanaoweza kuhudumiwa kwa siku.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment