
Mkuu wa Idara ya Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Deo Fazah akipokea zawadi alipotembelea banda la TET ndani ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es salaam (Sabasaba)2026.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Deo Fazah akizungumza alipotembelea banda la TET ndani ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es salaam (Sabasaba)2026.
……..
MKUU wa Idara ya Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Deo Fazah amesema taasisi hiyo ndiyo moyo halisi wa elimu Nchini kwa elimu yetu ya Msingi, elimu ya Sekondari na Ualimu.
Deo Fazah amesema hayo katika Banda la TET ndani ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea barabara ya Kilwa, Temeke Jijini Dar es salaam.
Amebainisha:”Tunapopata nafasi kama hii, tunashiriki ili kuwaambia Watanzania kile tunachofanya, tunapenda kuwakaribisha wadau wote wanaoweza kujitokeza Kufanya kazi na TET katika uandaaji wa Vitabu vya Kiada.
Pia Vitabu vyote vya Kiada vilivyofanyiwa maboresho tunavyo hapa na maeneo yote.
Taasisi ipo na maduka yake Kikanda, ikiwemo pale Ofisi TET Bamaga, lakini pia Kariakoo na kwa mawakala wengine wote.
Pia tupo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Kusini kote huko vitabu vyote vipo na vinauzwa kwa bei elekezi kwa bei ileile ambayo kitabu kinachouzwa Dar es salaam na Kigoma ama Mbeya kitauzwa kwa bei ileile,” Amesema Deo Fazah.
Aidha, amewakaribisha wadau wanaotaka kufanya masuala ya Utafiti katika elimu milango ipo wazi katika mashirikiano na TET katika kuendeleza elimu nchini.
Wazazi, walezi, Wanafunzi na wadau karibuni sana Vitabu vya kidato cha Tano na Sita pia vipo hapa na wote wanaweza kutembelea hapa Sabasaba lakini pia katika ofisi zetu za makao makuu ya TET
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment