

Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai CP Shabani Hiki, akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Hati ya Shukrani kutoka Umoja wa Vijana wenye Ualbino Tanzania (TYAF) ambapo amesema Jeshi la Polisi limepokea Hati hiyo kama utambuzi wa kazi inayofanywa kila siku na Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi kote nchini.
……….
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amesema, Usalama wa watu hauamuliwi kwa rangi ya ngozi yake, uraia, hali yake ya kiuchumi, kiafya au kijinsia kwani kwa Jeshi la Polisi, kila mtu ana haki sawa ya kuishi kwa amani, usalama na bila kutwezwa utu wake na ndiyo sababu Jeshi la Polisi linaendelea kulinda haki za kila mwananchi bila ubaguzi, wakiwemo watu wenye ualbino, wanawake, watoto, wazee na makundi mengine yote yaliyo katika mazingira hatarishi kwa wakati husika.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, leo Agosti 6,2026 Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai CP Shabani Hiki, wakati akipokea Hati ya Shukrani kutoka Umoja wa Vijana wenye Ualbino Tanzania (TYAF) amesema, Jeshi la Polisi limepokea Hati ya Shukrani kwa heshima na unyenyekevu mkubwa na imepokelewa si kama heshima kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi pekee, bali kama utambuzi wa kazi inayofanywa kila siku na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi kote nchini.
Aidha, Kamishna Hiki, ameeleza kuwa, kazi ya kulinda usalama wa raia na mali zao ni wajibu tuliopewa na Katiba na Sheria za nchi, ni dhamana tuliyoapa kuitekeleza kwa uadilifu, weledi na bila ubaguzi wa aina yoyote na kwamba kukabidhiwa kwa hati hiyo ya shukrani ni ishara ya kuendelea kutambuliwa kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na kutekelezwa na Jeshi la Polisi.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wenye Ualbino Tanzania (TYAF) ndugu Masoud Shaban, amesema kuwa, wamekabidhi Hati ya Shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kama ishara ya heshima, kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Amesema, hati hiyo ya shukrani ni sauti ya mioyo yao ambayo wameitoa kwa lengo la kujenga upya dhamira ya uhusiano na mashirikiano ya kimkakati baina ya Jeshi la Polisi na Umoja huo sambamba na kutambua juhudi kubwa zilizofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa matukio ya ukatili kwa watu wenye ualibino.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment