Na, Egidia, Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Kituo cha Afya cha ADN CARE ARUSHA kinachotoa huduma za afya za kibingwa kimejitolea kuhudumia wananchi bure katika maonyesho ya Nanenane yaliyoanza Leo 1August, 2026 na kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde.
Dr.Mapunda akizungumza na chombo hiki katika banda lake la kutolea huduma za afya, katika viwanja vya Nanenane, Njiro Arusha, amewakaribisha wananchi wote waliopo katika viwanja hivyo kusogea kupima afya zao bure.
Aidha ametaja huduma zinazotelewa kuwa ni pamoja na huduma ya macho, meno, kupima shinikizo la damu, sukari, kaswende, UKIMWI na vipimo vingine vya kibingwa na nyinginezo nyingi.
Hata hivyo amesisitiza wananchi kuwa na tabia ya kupima afya mara Kwa mara na si kusubiri hali kuwa ngumu. Amesema ADN CARE wamejiandaa kikamilifu kuhudumia wananchi Kwa siku nane na gari la kisafirisha wagonjwa lipo.
Kwa upande wake Mtaalam wa Maabara Festo Mmasy amesema wapo tayari kuhudumia wananchi wote watakaojiotokeza kupima afya zao.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment