Halmashauri ya Mji Kasulu imefanikiwa kuandaa Bonanza la Michezo lililozikutanisha Halmashauri tatu za Mkoa wa Kigoma ikiwemo Kasulu TC, Kasulu DC na Buhigwe DC ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2026 sambamba na safari ya kuelekea Jijini Mbeya kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA.Bonanza hili limefanyika tarehe 01 Agosti 2026 katika viwanja vya chuo cha ualimu Kasulu.Akizungumza wakati wa kufungua Bonanza hilo Afisa Utamaduni na Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Daud Schinga amesema michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano huku akiwataka watumishi wote wa Halmashauri hizo kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi.Michezo iliyochezwa ni Mpira wa Miguu vijana ambapo Kasulu TC imetoshana nguvu kwa kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya Buhigwe DC , mpira wa wavu (volleyball) Kasulu TC imepoteza kwa Set 2-0 dhidi ya Buhigwe DC.Michezo mingine ni Mpira wa miguu Veterani Kasulu TC imepoteza kwa goli 3-0 dhidi ya majirani zake Kasulu DC na mpira wa pete (netball) ikimalizia kwa Kasulu TC kupoteza kwa goli 20- 17 dhidi ya Buhigwe DC.Halmashauri ya Mji Kasulu inawapongeza washindi wote wa michezo hiyo na kuwakumbusha wananchi kuendelea kujiandaa kwa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, utakaowasili tarehe 10 Septemba 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment