Na Mapuli Kitina Misalaba
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia sekta ya Afya imeadhimisha wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa kuwataka wananchi, waajiri na wadau mbalimbali kushirikiana kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha akina mama kunyonyesha watoto wao ipasavyo ili kuboresha afya na maendeleo ya watoto.
Wito huo umetolewa leo katika Kituo cha Afya Kambarage wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 7, 2026, chini ya kaulimbiu isemayo "Mwanzo Imara wa Maisha ya Mtoto, Huanza na Maziwa ya Mama."
Akizungumza mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mary Makka, amesema unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni msingi muhimu wa kuhakikisha mtoto anakuwa na afya njema, kinga dhidi ya magonjwa na ukuaji bora wa mwili na akili.
Amesema jamii ina wajibu wa kuhakikisha mama anayenyonyesha anapata lishe bora, muda wa kutosha wa kunyonyesha, msaada wa kifamilia pamoja na mazingira rafiki nyumbani na sehemu za kazi ili kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo wa maisha ya mtoto.
Awali, akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Lishe wa Manispaa ya Shinyanga, Misango Andrea George, amesema maadhimisho hayo yameambatana na utoaji wa elimu ya lishe na unyonyeshaji kwa wazazi na walezi, upimaji wa hali ya lishe kwa watoto, matibabu kwa watoto wenye utapiamlo pamoja na ushauri wa kitaalamu kwa wajawazito na akina mama wanaonyonyesha.
Amesema kampeni ya uhamasishaji iliyoanza Agosti 1 imelenga kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa elimu na huduma za afya ili kuhakikisha watoto wanapata mwanzo bora wa maisha kupitia unyonyeshaji sahihi na lishe bora.
Community Health Coordinator/Project Manager kutoka shirika la Doctors with Africa CUAMM, Henry Mosabi ametoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).
Mkuu wa Kitengo cha Kliniki ya Mama, Baba na Mtoto katika Kituo cha Afya Kambarage, Rose Mbigule, ametoa elimu kuhusu unyonyeshaji sahihi wa watoto, akiwahimiza akina mama kuanza kunyonyesha watoto wao ndani ya saa moja baada ya kujifungua.
Sambamba na elimu hiyo, washiriki wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa chakula bora na chenye lishe kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao.
Wataalamu wa lishe wametoa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia makundi sita ya vyakula ili kuhakikisha wajawazito, akina mama wanaonyonyesha na watoto wanapata virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji na afya bora na kwamba washiriki pia wameelekezwa namna ya kuandaa mlo kamili kwa gharama nafuu kwa kutumia mazao yanayopatikana katika jamii.
Baadhi ya wajawazito na akina mama wenye watoto chini ya miaka mitano ambao wameshiriki mafunzo hayo wameishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia sekta ya afya pamoja na wadau wa afya kwa kuwapatia elimu hiyo, wakisema imewasaidia kuongeza uelewa kuhusu unyonyeshaji, lishe bora na malezi ya watoto.
Wameahidi kwenda kutumia maarifa waliyoyapata katika familia zao na kuyasambaza kwa wanawake wengine katika maeneo wanayoishi ili kuchangia kupunguza utapiamlo na kuboresha afya ya mama na mtoto.
Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani huadhimishwa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi 7 kwa lengo la kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama katika kuboresha afya ya mama na mtoto pamoja na kupunguza utapiamlo na vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika.
Akizungumza mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mary Makka, amehimiza jamii kuweka mazingira wezeshi kwa akina mama wanaonyonyesha.
Afisa Lishe wa Manispaa ya Shinyanga, Misango Andrea George, awali akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Kambarage.
Kaimu mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga, Antony Mwampulo akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mtendaji wa kata ya Kambarage Sara Wamkury, akizungumza.
Akizungumza mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mary Makka, amehimiza jamii kuweka mazingira wezeshi kwa akina mama wanaonyonyesha.
Akizungumza mgeni rasmi, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mary Makka, amehimiza jamii kuweka mazingira wezeshi kwa akina mama wanaonyonyesha.
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga (A/INSP) Happiness Mathias Madondola, akishiriki vema katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani.
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga (A/INSP) Happiness Mathias Madondola, akishiriki vema katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambayo katika Manispaa ya Shinyanga yamefanyika kwenye viwanja vya kituo cha afya Kambarage.

Washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani wakifuatilia mada mbalimbali kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama, lishe bora na afya ya mtoto.

Mkuu wa Kitengo cha Kliniki ya Mama, Baba na Mtoto katika Kituo cha Afya Kambarage, Rose Mbigule, akitoa elimu ya unyonyeshaji sahihi wa maziwa ya mama kwa wajawazito na akina mama wenye watoto wadogo.

Community Health Coordinator/Project Manager kutoka Doctors with Africa CUAMM, Henry Mosabi, akitoa elimu kuhusu kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU).
Baadhi ya wajawazito na akina mama wenye watoto chini ya miaka mitano wakishiriki mafunzo ya lishe na unyonyeshaji katika Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani.
Mratibu elimu ya afya kwa umma Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula akitoa elimu katika maadhimisho hayo.

Community Health Coordinator/Project Manager kutoka Doctors with Africa CUAMM, Henry Mosabi, akitoa elimu kuhusu kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU).SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment