Kijana Edzani Bakoba Mzaliwa wa mkoa wa Kigoma anaeishi na kufanya biashara ya machinga katika Stendi ya zamani iliyopo wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga amewataka vijana wenzake kutokuchagua badalayake kuchangamkia fulsa zilizopo katika jamii.
Kijana huyo ameyazungumza hayo leo Agost 11,2026 ikiwa ni siku ya Vijana kimataifa akibainisha kunufaika na biashara hiyo kwa kupata pesa ya kumudu gharama za maishayake na familia yake.
Kijana huyo amesema kwa zaidi ya miaka minne amekuwa akifanya shughulizake ndani ya stendi hiyo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wateja jambo lililompa manufaa kwa kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo Saa,kofia,Pamoja na vipodozi kwa wanawake.
Sambamba na hilo kijana huyo amesema licha ya changamoto mbalimbali hususani wakati wa kipindi cha masika malengoyake ni kupiga hatua kubwa katika shughuli hiyo kwa kufungua duka kubwa la mahitaji mbalimbali.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment