Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Ilala Bw. Musibu Shabani amesema kuwa TRA imejidhatiti kuhakikisha biashara zinakua kwa kukusanya kodi bila kuziathiri ukuaji biashara hizo.

Bw. Shabani ameyasema hayo leo tarehe 06 Agosti, 2026 wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Mtaa wa Kitonga, Kata ya Msongola iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa biashara ndiyo chanzo kikuu cha kodi ambazo ndiyo mhimili wa maendeleo na kujitegemea kwa taifa hivyo ni jukumu la TRA kuzilinda biashara na kuhakikisha zinakua.

“Biashara na kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu. Tunaendelea kuimarisha ukaribu kwa kusikiliza changamoto zenu na kuzitatua ili ulipaji na ukusanyaji wa kodi usiwe kizuizi kwa biashara kustawi,” amesema Bw. Shabani.

Aidha, amewasisitiza wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kikodi ikiwemo kujisajili na kupata TIN, kufanya makadirio na kulipa kodi stahiki kwa wakati.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wameipongeza TRA kwa kutenga siku ya Alhamisi kwa viongozi kusikiliza changamoto za walipakodi moja kwa moja, huku wakisifu ukaribu uliopo sasa baina ya TRA na walipakodi.

   SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254