Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, ameridhishwa na ubunifu wa teknolojia, ubora wa bidhaa na mpangilio wa Banda la Halmashauri hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yanayoendelea katika Viwanja vya Ipuli, Manispaa ya Tabora.Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mwl. Simbeye amesema maonesho hayo yanaakisi kaulimbiu ya mwaka 2026 ya "Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," kupitia ubunifu wa teknolojia, ubora wa bidhaa na elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi.Mwl. Simbeye ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwezesha wananchi kupitia mikopo ya asilimia 10, akisema hatua hiyo imeongeza fursa za ajira, imechochea ubunifu wa teknolojia na kuimarisha shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na ujasiriamali."Napenda kuishukuru Serikali chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha mikopo asilimia kumi kwa sababu nimepita katika Banda letu na kujionea vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo vikifanya vizuri sana na kuona tija kwetu sisi Halmashauri kuendelea kuyawezesha makundi hayo kupitia mikopo hiyo"Aidha, amewashukuru viongozi, wadau na wananchi wote waliotembelea Banda la Halmashauri ya Mji Kasulu, huku akiwahimiza ambao bado hawajafika kutumia fursa hiyo kujionea teknolojia mbalimbali, bidhaa bora na mbinu bunifu zinazochochea maendeleo ya kiuchumi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment