" MVULI ESTATES YAONGEZA KASI YA MAENDELEO WILAYA YA ARUSHA.

MVULI ESTATES YAONGEZA KASI YA MAENDELEO WILAYA YA ARUSHA.

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

Kampuni ya Mvuli Estates Company Limited, inayomiliki hoteli za kitalii jijini Arusha na wilayani Karatu, imeendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo miundombinu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jonathan Ogillo, amesema kampuni imewekeza katika miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kushirikiana na serikali za mitaa na wadau wengine wa maendeleo.

Amesema miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni ufungaji wa taa za barabarani ili kuongeza usalama kwa wananchi na watumiaji wa barabara, hususan nyakati za usiku.

Aidha Ogillo amesema kuwa kampuni imejenga barabara ya ndani yenye urefu wa mita 114 kutoka eneo la Kwa-shabani hadi hoteli ya Mvuli kwa kiwango cha zege, hatua iliyoboresha usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

Ameeleza kuwa uwekezaji huo unaonesha dhamira ya kampuni katika kurudisha sehemu ya faida kwa jamii kupitia miradi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji wengine kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo, akisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma una mchango mkubwa katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.

"

Maendeleo ya kweli yanaanza na mtu mmoja mmoja, sio lazima kusubiri serikali, hivyo kujitoa na ushirikiano unachangia kuharakisha maendeleo katika jamii," amesema Ogillo.

Kutokana na hatua hiyo ametoa mfano wa namna sekta binafsi inavyoweza kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo endelevu nchini.

 Aidha Ogillo amesema kuwa kampuni imejenga barabara ya ndani yenye urefu wa mita 114 kutoka eneo la Kwa-shabani hadi hoteli ya Mvuli kwa kiwango cha zege, hatua iliyoboresha usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

Ameeleza kuwa uwekezaji huo unaonesha dhamira ya kampuni katika kurudisha sehemu ya faida kwa jamii kupitia miradi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji wengine kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo, akisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma una mchango mkubwa katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.

"Maendeleo ya kweli yanaanza na mtu mmoja mmoja, sio lazima kusubiri serikali, hivyo kujitoa na ushirikiano unachangia kuharakisha maendeleo katika jamii," amesema Ogillo.

Kutokana na hatua hiyo ametoa mfano wa namna sekta binafsi inavyoweza kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo endelevu nchini.

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa kutambua mchango  na umuhimu wa Mvuli Estates Company Limited katika maendeleo ya jamii, imetoa cheti cha kutambua mchango wa kampuni hiyo na kuishukuru kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha na matengenezo ya miundombinu.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Suleiman Msumi wakati akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Jonathan Ogillo ameipongeza Kampuni hiyo Kwa ushirikiano mkubwa na kuunga mkono juhudi za serikali. Amesema wawekezaji wa ndani  waige mfano wake Ili kuchochea maendeleo ya jamii.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post