" MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA TPBA KUWA WABUNIFU NA KUZINGATIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MSINGI

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AWATAKA TPBA KUWA WABUNIFU NA KUZINGATIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MSINGI


Na,Egidia Vedasto, Misalaba Media Arusha.Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari, amekitaka Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kuwa wabunifu na kujikita katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi, akisisitiza kuwa wananchi na Taifa wanawategemea katika kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi.Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na  Uongozi mpya wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), walipomtembelea na kujitambulisha rasmi, trh 4 Agosti, 2026 Ofisi Ndogo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  jijini Dar es Salaam. Aidha Mhe.Johari amesema TPBA kina wajibu mkubwa wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, huku akisisitiza umuhimu wa kutoa ufafanuzi kuhusu upotoshaji unaofanyika katika mitandao ya kijamii, akieleza kuwa bila kufanya hivyo, jamii inaweza kufanya maamuzi kutokana na taarifa zisizo sahihi.Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), Bw. Bonaventure Mwambaja ameahidi kuwa uongozi wake utatekeleza kwa vitendo mpango kazi uliowekwa ili kuhakikisha chama kinaendelea kutoa huduma bora kwa Taifa.Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kililenga kuutambulisha rasmi uongozi mpya wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kwa mlezi wao, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, pamoja na kuwasilisha mpango kazi wao wa utekelezaji wa majukumu ya Chama.Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali aliambatana na Viongozi wengine wa Chama hicho akiwemo Makamu wa Rais, Bw. Acley Chaule, Mwenyekiti Bi. Selestina Kunambi, na Makamu Mwenyekiti Bi. Farida Kiobya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post