" MZEE BOAZ DAUD TUNGU AZIKWA SHINYANGA, AACHA WATOTO 24 NA WAJUKUU 122

MZEE BOAZ DAUD TUNGU AZIKWA SHINYANGA, AACHA WATOTO 24 NA WAJUKUU 122

MZEE BOAZ AZIKWA LEO SHINYANGA

Mazishi ya Mzee Boaz Daud Tungu, aliyefahamika na wengi kwa kujichimbia kaburi lake zaidi ya miaka nane kabla ya kufariki dunia, yamefanyika leo Agosti 2, 2026 katika Mtaa wa Ndembezi, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Akisoma historia ya maisha ya marehemu wakati wa ibada ya mazishi, mjukuu wake, Bi. Iline Edward, amesema Mzee Boaz alizaliwa Aprili 13, 1929 katika Kijiji cha Nyandekwa Busiya, Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.

Amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na kwamba Julai 30, 2026 majira ya saa Nane usiku alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 97.

Kwa mujibu wa historia hiyo, Mzee Boaz ameacha watoto 24, wajukuu 122, vitukuu 139 pamoja na vilembwe watano, huku akiacha kumbukumbu ya maisha yenye mafundisho na upendo kwa familia yake.

Akizungumza kwa niaba ya familia, mtoto wa nne wa marehemu, Robert Boaz, ambaye aliwahi kulitumikia Jeshi la Polisi Tanzania katika nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Kamanda wa Polisi katika mikoa kadhaa na baadaye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini, amewashukuru ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote walioshiriki katika kipindi chote cha kuuguza, kuomboleza na hatimaye kumpumzisha baba yao.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post