" NUZULACK DAUSSEN AMPONGEZA MAPULI MISALABA KWA UBUNIFU WA SHY TALENT FILMS

NUZULACK DAUSSEN AMPONGEZA MAPULI MISALABA KWA UBUNIFU WA SHY TALENT FILMS

Mkufunzi wa mafunzo ya mameneja wa vituo vya Radio mikoa mitatu ya kanda ya Ziwa Nuzulack Daussen ambae pia ni Mtendaji wa Taasisi ya Nukta Afrika amempongeza ripota wa Gold Fm manispaa ya Shinyanga Mapuli Misalaba kwa utengenezaji wa maudhui ya uigizaji (SHY TALENT FILMS) ambayo amesema huenda yakamuongezea mapato siku zijazo

Ripota huyo anaemiliki Misalaba Media amepongezwa kwa ubunifu wa maudhui hayo ambayo mkufunzi huyo amesema Yana maslahi katika Dunia hii ya teknolojia.

Akizungumza katika mafunzo ya mameneja wa vituo vya Radio mikoa mitatu ya kanda ya Ziwa ambayo ni Shinyanga,Mwanza na Geita amesema Dunia ya teknolojia bila kuwa mbunifu wa maudhui na kutumia platform za dijitali unaweza usifikie malengo.

Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania Kanda ya Ziwa ni ya kuwawezesha mameneja wa vituo vya Radio katika mikoa hiyo mitatu kujitegemea na kutengeneza mapato zaidi.

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum Banali akifungua mafunzo hayo amesema ni wajibu wa kila kituo cha utangazaji kuwapatia mafunzo staff wao ambapo amesema hilo ni takwa la kisheria katika utangazaji.

Katika mafunzo hayo mameneja wa vituo vya Radio kutoka mikoa hiyo mitatu pia walijifunza kutengeneza mipango kazi katika vyumba vya habari,kutumia platform za dijitali kuongeza mapato na kutengeneza mpango kazi katika biashara.

Mameneja hao pia walitumia nafasi hiyo kujadili changamoto mbalimbali katika eneo la biashara na maudhui.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA


 

Post a Comment

Previous Post Next Post