KAMPUNI cha Radiant ya mkoani Pwani imesambaza mafuta ya lotion box 1000 bure kwenye maonesho ya Nanenane jijini Mwanza kutangaza bidhaa zake mpya aina ya Tulip Grow inayotengenezwa hapa nchini.
Akizungumza katika ugawaji wa bidhaa hiyo kwa wananchi mbalimbali waliofurika katika banda la kampuni hiyo leo jijini hapa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Shaik Khoja alisema wameamua kugawa lotion hizo bure ili kuwafanya watumiaji kufahamu bidhaa hiyo.
Alisema sambamba na kutangaza bidhaa hizo kwa kuwagawia watu waliofika kwenye maonesho hayo lakini vilevile ni njia mojawapo ya kuwafanya watu washerekee kwa furaha.
Kampuni inatengeneza bidhaa aina ya Body lotion, Body cream, Petroleum Jelly, Shampoo na bidhaa zingine mbalimbali kwa kutumia malighafi za hapa nchini.
Alisema kuwa Radiant Industries Ltd ipo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani inazalisha bidhaa hizo kwa kiwango cha ubora utakiwao na Taasisi ya Viwango Tanzania (TBS).
Baadhi ya wananchi waliopata bidhaa hizo Benedetha Dwasi toka Igoma jijini Mwanza alishukuru kupata.mafuta na kuahidi kuanza kuyatumia.
Mary Michael wa Igoma alisema kwa sasa kumekuwa na matumizi ya mafuta ya vipodozi yenye madhara usoni hivyo kuomba kuwepo na ukaguzi kubaini ubora

Post a Comment