" TANZANIA YAJIIMARISHA MATUMIZI YA AKIKI UNDE KATIKA UTAHINI.

TANZANIA YAJIIMARISHA MATUMIZI YA AKIKI UNDE KATIKA UTAHINI.


Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli za utahini, hatua inayolenga kurahisisha ufundishaji na kuboresha mchakato wa upimaji na tathmini ya wanafunzi.

Prof. Nombo amesema maendeleo ya teknolojia yameleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu, akieleza kuwa Tanzania inajivunia hatua iliyofikiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika kuanza kutumia akili unde (Artificial Intelligence) katika shughuli za utahini na kufanya tathmini.

Amesema hayo katika mkutano wa 42 wa shirikisho la mabaraza ya mitihani Afrika (AEAA) uliofanyika Jijini Arusha na kubainisha kuwa matumizi ya akili unde yanaweza kuongeza ufanisi katika upimaji na tathmini, hivyo Serikali itaendelea kuhimiza matumizi sahihi ya teknolojia katika elimu ili kuendana na mabadiliko ya dunia ya kidijitali.

 "Kuna umuhimu wa kuwa makini, kwa kuwa pamoja na manufaa yake, teknolojia hiyo inaweza kuleta madhara iwapo haitatumika kwa kuzingatia maadili, usalama wa taarifa na taratibu zinazofaa"

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt. Said Mohamed, amesema Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 42 wa Shirikisho la Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), unaolenga kujadili mabadiliko ya kiteknolojia katika mifumo ya elimu na mitihani barani Afrika.


Dkt. Said amesema moja ya ajenda kuu za mkutano huo ni kujadili matumizi ya akili unde katika elimu, hususan katika upimaji na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kuchambua faida na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo.

Vilevile amefafanua kuwa, mifumo mingi ya elimu na uendeshaji wa mitihani kwa sasa inategemea maendeleo ya teknolojia, hivyo mkutano huo utatoa fursa kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali kujadili namna akili unde inavyoweza kutumika kuboresha upimaji, utahini na utoaji wa huduma za elimu

"Usalama wa mitihani ni miongoni mwa masuala muhimu yatakayojadiliwa, ikiwemo namna ya kutumia teknolojia kuhakikisha mitihani inalindwa dhidi ya udanganyifu na changamoto nyingine zinazoweza kujitokeza katika mifumo ya kidijitali".

DR. Said ameongeza kwamba Tanzania inaendelea kuelekea katika matumizi makubwa ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kijamii, huku akieleza kuwa ifikapo mwaka 2050, inatarajiwa asilimia 80 ya huduma zote za kijamii zitakuwa zikitolewa kupitia mifumo ya TEHAMA.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post