Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika la Green Community Initiatives (GCI), kwa
kushirikiana na Restless Development, limetoa mafunzo ya uraia kwa vijana 50
kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa Mradi wa AU-EU Youth Voice Lab, unaolenga kuwajengea vijana uwezo wa
kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii, kiutawala na maendeleo ya
jamii.
Katika mafunzo hayo, vijana wamefundishwa kuhusu dhana
ya uongozi, aina za uongozi na sifa muhimu anazopaswa kuwa nazo kiongozi
anayelenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mwakilishi wa shirika la Restless Development Cecilia
Msangwa kutoka shirika la YAWE ambaye alikuwa sehemu ya wawezeshaji katika mafunzo
hayo ameeleza kuwa uongozi haupaswi kuhusishwa pekee na mtu anayeshika nafasi
rasmi ya kisiasa au kiutawala, bali kila kijana ana nafasi ya kuwa kiongozi
katika jamii yake kwa kuanzisha mawazo mapya, kuhamasisha wengine na kushiriki
katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi.
Vijana pia wamepewa uelewa kuhusu umuhimu wa kuwa na
viongozi wenye maono, wanaowajibika na wanaoweza kusikiliza mahitaji ya
wananchi huku wakihimizwa kutumia nafasi walizonazo kushiriki katika shughuli
za maendeleo badala ya kusubiri kupewa nafasi za uongozi.
Peter Joseph kutoka Shirika la YAWE, ambaye naye alishiriki
kwa niaba ya Restless Development amewasilisha mada mbalimbali ikiwemo uwajibikaji,
ambapo vijana wameelezwa kuwa raia wana wajibu wa kufuatilia na kuelewa namna
shughuli za maendeleo zinavyotekelezwa katika maeneo yao.
Katika sehemu ya utafiti, washiriki wamefundishwa
umuhimu wa kukusanya taarifa sahihi kabla ya kufanya maamuzi au kutoa hoja
kuhusu jambo lolote linalohusu jamii.
Mada ya ushawishi pia imepewa nafasi katika mafunzo
hayo, ambapo vijana wamefundishwa namna ya kutumia hoja, ushahidi na njia
mbalimbali za mawasiliano kushawishi mabadiliko chanya katika jamii.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salome Komba, ameyapongeza mashirika ya
GCI na Restless Development kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema kuwa vijana ni
sehemu muhimu ya jamii na wanapaswa kupewa nafasi na maarifa yatakayowawezesha
kushiriki katika maendeleo.
Salome amewasisitiza vijana kutumia elimu waliyoipata
katika mafunzo hayo kwa vitendo, hususan kwa kushiriki katika shughuli za
kijamii, kufuatilia masuala yanayowahusu na kutoa mawazo yanayoweza kusaidia
kuboresha maisha ya wananchi.
Naye Afisa Vijana wa Manispaa ya Shinyanga, Enea
Boniface, amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia fursa za mafunzo kama hayo
kujenga uwezo wao na kuongeza ushiriki wao katika masuala ya maendeleo.
Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Maryciana William
kutoka Shirika la Green Community Initiatives (GCI), amesema lengo la mafunzo
hayo ni kuwajengea vijana uelewa na uwezo wa kutumia maarifa waliyopewa katika
kushiriki kwenye mijadala na shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo ya jamii.
Amesema GCI imekuwa ikitambua umuhimu wa vijana katika
kujenga jamii yenye ushiriki, uwajibikaji na maendeleo, hivyo mafunzo hayo
yameandaliwa ili kuwapa vijana maarifa ambayo wataweza kuyatumia katika maeneo
yao.
Baadhi ya vijana walioshiriki katika mafunzo hayo,
akiwemo Emmanuel Robert, Mhoja Ibengwe, Eliya Bahame na Neema Songela,
wameyashukuru mashirika ya GCI na Restless Development kwa kuwapa nafasi ya
kupata elimu zaidi kuhusu masuala ya uraia na uongozi.
Aidha, wameahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa
kuwafikishia vijana wengine elimu waliyoipata, ili maarifa hayo yasiishie kwa
washiriki 50 pekee, bali yaweze kuwafikia vijana wengi zaidi ndani ya Manispaa
ya Shinyanga.

Mwakilishi wa Shirika la Restless Development, Cecilia
Msangwa kutoka YAWE, akizungumza wakati wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga,
akisisitiza kuwa uongozi si lazima uhusishwe na mtu anayeshika nafasi rasmi ya
kisiasa au kiutawala, bali kila kijana ana nafasi ya kuwa kiongozi katika jamii
yake.

Vijana 50 wakishiriki mafunzo ya uraia yaliyoandaliwa na GCI kwa kushirikiana na Restless Development, wakijengewa uwezo katika uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Cecilia Msangwa akiwahimiza vijana kutumia uwezo na nafasi walizonazo kuanzisha mawazo mapya, kuhamasisha wengine na kushiriki katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi.
Peter Joseph kutoka Shirika la YAWE, akitoa mada
kuhusu uwajibikaji wakati wa mafunzo, akiwafundisha vijana umuhimu wa
kufuatilia na kuelewa namna shughuli za maendeleo zinavyotekelezwa katika
maeneo yao.

Peter Joseph kutoka Shirika la YAWE, akitoa elimu
kuhusu ushawishi, ambapo vijana wamefundishwa namna ya kutumia hoja, ushahidi
na njia sahihi za mawasiliano kushawishi mabadiliko chanya katika jamii.

Afisa Vijana wa Manispaa ya Shinyanga, Enea Boniface,
akizungumza na vijana wakati wa mafunzo hayo, akiwahimiza kutumia fursa kama
hizo kujenga uwezo wao na kuongeza ushiriki katika masuala ya maendeleo ya
jamii.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga, Salome Komba, akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kupongeza GCI na
Restless Development kwa kuwawezesha vijana, huku akiwataka washiriki kutumia
elimu waliyoipata katika shughuli za maendeleo ya jamii.
Washiriki wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga wakifanya kazi kwa pamoja katika vikundi, wakijadili mada mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Mafunzo yakiendelea mjini Shinyanga, vijana wakipata elimu na ujuzi wa kutumia sauti zao kushiriki katika masuala ya maendeleo na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Washiriki wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga wakifanya kazi kwa pamoja katika vikundi, wakijadili mada mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Washiriki wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga wakifanya kazi kwa pamoja katika vikundi, wakijadili mada mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Mafunzo yakiendelea mjini Shinyanga, vijana wakipata elimu na ujuzi wa kutumia sauti zao kushiriki katika masuala ya maendeleo na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Afisa Vijana wa Manispaa ya Shinyanga, Enea Boniface,
akizungumza na vijana wakati wa mafunzo hayo, akiwahimiza kutumia fursa kama
hizo kujenga uwezo wao na kuongeza ushiriki katika masuala ya maendeleo ya
jamii.
Enea Boniface akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kuendelea kujifunza na kuongeza maarifa katika maeneo mbalimbali ili waweze kushiriki kikamilifu katika uongozi na shughuli za maendeleo.
Afisa Vijana wa Manispaa ya Shinyanga, Enea Boniface,
akizungumza na vijana wakati wa mafunzo hayo, akiwahimiza kutumia fursa kama
hizo kujenga uwezo wao na kuongeza ushiriki katika masuala ya maendeleo ya
jamii.

Mafunzo ya AU-EU Youth Voice Lab yakiendelea mjini
Shinyanga, yakitoa nafasi kwa vijana kujifunza, kujadili na kubadilishana
mawazo kuhusu masuala yanayogusa jamii.

Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Peter Joseph kutoka Shirika la YAWE, akitoa mada
kuhusu uwajibikaji wakati wa mafunzo, akiwafundisha vijana umuhimu wa
kufuatilia na kuelewa namna shughuli za maendeleo zinavyotekelezwa katika
maeneo yao.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Peter Joseph kutoka Shirika la YAWE, akiwajengea
vijana uelewa kuhusu umuhimu wa kukusanya na kutumia taarifa sahihi kabla ya
kufanya maamuzi au kutoa hoja zinazohusu jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Maryciana William kutoka Shirika la Green Community
Initiatives (GCI) akizungumza wakati wa mafunzo.
Washiriki wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga wakifanya kazi kwa pamoja katika vikundi, wakijadili mada mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Wawakilishi wawili kutoka Kundi la vijana wakiwasilisha
mbele ya wenzake matokeo ya mjadala wa kikundi, akieleza hoja zilizojadiliwa
wakati wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga.

Washiriki wakiandika hoja na majibu ya mijadala ya vikundi wakati wa mafunzo ya uraia, huku wakitumia maarifa na uzoefu wao kujenga uelewa wa pamoja.

Wawakilishi wawili kutoka Kundi la vijana wakiwasilisha mbele ya wenzake matokeo ya mjadala wa kikundi, akieleza hoja zilizojadiliwa wakati wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Viongozi na wawakilishi kutoka mashirika yaliyoshirikiana katika mafunzo hayo wakiwa ndani ya ukumbi, wakifuatilia kwa karibu mijadala na uwasilishaji wa vijana wakati wa mafunzo ya uraia mjini Shinyanga.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.

Vijana 50 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya
Shinyanga wakiendelea kupata mafunzo ya uraia yanayolenga kuwaongezea uelewa
kuhusu uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Mafunzo ya uraia kwa vijana yakiendelea mjini Shinyanga, ambapo washiriki wanajengewa uwezo wa kutambua nafasi yao katika uongozi, uwajibikaji na maendeleo ya jamii.
Cecilia Msangwa akiwahimiza vijana kutumia uwezo na nafasi walizonazo kuanzisha mawazo mapya, kuhamasisha wengine na kushiriki katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi.
Vijana 50 wakishiriki mafunzo ya uraia yaliyoandaliwa na GCI kwa kushirikiana na Restless Development, wakijengewa uwezo katika uongozi, uwajibikaji, utafiti na ushawishi.
Cecilia Msangwa akiwahimiza vijana kutumia uwezo na nafasi walizonazo kuanzisha mawazo mapya, kuhamasisha wengine na kushiriki katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi.
Vijana, wawezeshaji pamoja na viongozi na wawakilishi wa mashirika yaliyoshiriki katika mafunzo ya uraia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo mjini Shinyanga.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment