" TANZANIA YAZINDUA JUKWAA LA NANE LA WADAU WA MAENDELEO YA BONDE LA MTO NILE

TANZANIA YAZINDUA JUKWAA LA NANE LA WADAU WA MAENDELEO YA BONDE LA MTO NILE

  Jukwaa la Nane la Wadau wa Maendeleo ya Bonde ya Mto Nile (NBDF8) limezinduliwa rasmi nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefanya uzinduzi huo jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Maji.

Lengo la jukwaa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa nchi washirika wa Bonde la Mto Nile katika kutafuta suluhisho bunifu za kugharamia miundombinu ya maji na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mhandisi Mwajuma amesema Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa jukwaa akisisitiza kuwa Tanzania ni mshirika muhimu katika bonde hilo hasa kutokana na ukweli kuwa Mto Nile chanzo chake kikubwa ni ziwa Victoria ambalo sehemu yake ipo Tanzania

Ameeleza kuwa Bonde la Mto Nile linakabiliwa na changamoto zinazoongezeka kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la idadi ya watu na matumizi, ukuaji wa uchumi pamoja na mahitaji makubwa ya maji, chakula na nishati. 

Ukuaji huo unasukuma umuhimu wa nchi wanachama kushirikiana katika kulinda, kuendeleza na kusimamia rasilimali za maji zinazoshirikishwa.

Ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushiriki wa Tanzania katika Bonde hilo kuwa ni pamoja na kuboreshwa kwa vituo vinane vya kitaifa vya ufuatiliaji wa taarifa za maji katika Bonde la Ziwa Victoria, matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano katika ukusanyaji wa taarifa za maji pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kufuatilia ubora wa maji, na maji chini ya ardhi, pamoja na nishati ya umeme.

Jukwaa hilo litatekelezwa kupitia shughuli mbalimbali zitakazojumuisha uwasilishaji wa tafiti, semina za mtandaoni, kampeni za uhamasishaji wa umma na mkutano wa mkuu utakaofanyika Dar es Salaam, ambapo itafanyika mijadala ya kitaalamu, majadiliano ya viongozi mbalimbali. Aidha amewaalika wataalamau wa maandiko na waandishi wa habari kushiriki kwa kuwasilisha habari na maandiko ambayo yatashindanishwa na kupata tuzo.

 Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Bonde la Nile Mhandisi Nestor Niyonzima ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki katika kuwasilisha maandiko na habari mbalimbali ambazo zinazohusu Bonde la Mto Nile kwa lugha mbalimbali, ikiwamo Kiswahili.          SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post