Serikali imeagiza vijana watumie teknolojia kwa busara ili kufungua milango ya fursa, kujenga ujuzi na kuchangia maendeleo ya taifa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la vijana lililofanyika mjini Dodoma kuadhimisha Siku ya Vijana ya Kimataifa, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa na nidhamu, uaminifu na utayari wa kujifunza kutokana na changamoto wanazokutana nazo.
Alieleza kuwa teknolojia, hasa akili unde, inaweza kutumika kama darasa, soko, ofisi na chombo cha kutatua changamoto badala ya kuwa njia ya kuacha kufikiri, huku akiwahimiza kijana mwenye nidhamu na utayari wa kujifunza kuweza kukua na kubadilika kiuchumi na kijamii.
Aidha, Omolo aliwasisitiza vijana kubadili mtazamo kuhusu ajira kwa kutambua kuwa kazi haipatikani katika sekta rasmi pekee, bali ipo pia katika kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, viwanda, teknolojia, sanaa, michezo, utalii na sekta nyingine nyingi.
Aliwataka wanaotafuta mikopo na fursa za biashara kujenga uwezo wa kuandika mipango thabiti ya biashara, kutunza kumbukumbu, kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa na kuheshimu makubaliano.
Aliwakumbusha pia kutopuuza afya zao, hususan kujiepusha na dawa za kulevya, kusimama imara dhidi ya shinikizo mbaya la rika, na kutooja kuomba msaada wanapokabiliwa na msongo wa mawazo au changamoto za afya ya akili, akisisitiza kuwa ujasiri wa kweli upo katika kulinda heshima na matarajio ya maisha yao.
Katika kuhitimisha, Omolo aliwasihi vijana kuonesha uzalendo kwa kufanya kazi kwa uaminifu, kuheshimu sheria, kulinda amani, kutunza mazingira na kukataa rushwa, chuki na ubaguzi.
Alibainisha kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, mikopo ya asilimia nne ya mapato ya ndani ya halmashauri, fursa za manunuzi ya umma na programu mbalimbali za kukuza ujuzi, huku Msaidizi wa Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Majaliwa Marwa akisisitiza kuwa maendeleo ya vijana hayawezi kutenganishwa na afya na ustawi wao kwa ujumla.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment