Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Wataalamu wa hesabu kutoka Afrika na Nchi za Nordic Japan, Sweden, na Norway wameketi Jijini Arusha katika mkutano wao wa pili kujadili kuhusu somo la hesabu.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Mgeni rasmi, Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar-es Salaam (UDSM) Prof. William Anangisye amesema mkutano huo unalenga kuwapa wataalamu hao changamoto katika kuimarisha ufundishaji wa hesabu Kwa wanafunzi wa ngazi ya Uzamili pamoja na kufanya tafiti.
Aidha amewataka wataalamu wa hesabu kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano katika tafiti na miradi mingine inayohusiana na hesabu ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji na matumizi ya taaluma hiyo Kwa maendeleo ya taifa.
"Hatua hii inatupa nafasi ya kuweka msisitizo wa somo la hesabu, kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya chini hadi elimu ya juu, msingi mzuri wa hesabu kwa wanafunzi ni muhimu katika kuwaandaa kwa taaluma mbalimbali zinazohitaji ujuzi wa kihisabati" amesema.
Vilevile Prof. Anangisye amesema kuwa hesabu ni eneo linalotakiwa kupewa kipaumbele Kwa umuhimu wake, kutokana na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini Tanzania, likisaidia kuzalisha walimu, wataalamu wa fedha, wachumi na wanasayansi.
Katika namna hiyohiyo Mratibu Msaidizi Idara ya Hesabu na Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar-es Salaam (UDSM)Dkt. Sylivesta Rugeiyhamu, amesema mkutano huo umewakutanisha wataalamu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia kujadili namna ya kuimarisha utafiti shirikishi katika hesabu na elimu ya hesabu kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu.
Ameongeza kuwa mkutano huo unalenga kuangalia kwa kina nafasi ya hisabati katika kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo, huku wataalamu wakibadilishana uzoefu, maarifa na matokeo ya tafiti zinazohusiana na taaluma hiyo.
"Mkutano huu pia unajadili matawi mbalimbali ya hesabu yanayohusisha sayansi na teknolojia, pamoja na matumizi ya akili mnemba (AI), ambayo kwa sasa yanaendelea kuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya taaluma na sekta mbalimbali"
Hata hivyo Dkt. Rugeihyamu amesema, mkutano umewakutanisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 30, huku lengo likiwa ni kuhakikisha somo la hisabati linapewa kipaumbele zaidi, linaendelezwa na kuwa kinara katika kuchangia maendeleo ya sayansi, teknolojia na maendeleo endelevu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment